Wakati wamemaliza mazoezi walipewa wasaa wa kuzunguka ndani ya klabu ila ndoto ya Mbappe ni kuonana na Cristiano Ronaldo, Zidane kamshika mkono Mbappe kuelekea ilipo timu ya wakubwa ili Kinda huyo aonane na Ronaldo.

Njiani Zizzou akiwa na Mbappe walikutana na Jorge Voldano moja kati ya viongozi wakubwa wa Real Madrid wakati huo, Zizzou alimuulizia kuhusu wakina Ronaldo, ila Voldano alimwambia wachezaji wameondoka tangu saa moja limepita kurudi kwao.
Mbappe aliumia sana, Zizzou aligundua hilo akamwambia basi twende mpaka vyumba vya kubadili nguo ukapaone tu Ronaldo anapokaa, lakini nitakupelekea La Finca (Mitaa anayoishi Ronaldo pale Jijini Madrid) kama yeye mwenyewe ataridhia, Zizzou aliendelea kumpanga Mbappe.
Walifika mpaka vyumbani lakini ajabu sana, Ronaldo anakuwa wa mwisho kuondoka mazoezini na anakuwa wa kwanza kuja, hivyo bahati nzuri hakuwa ameondoka bali alikuwa ametoka kuoga anajiandaa aondoke, ikawa bahati kwa Mbappe sasa.
Mkurugenzi wa Mahusiano na jamii Emiliano Butragueno alimsimamisha Ronaldo na kumwambia Zizzou anamtafuta sana, yupo na mtoto mdogo kutoka Paris anataka amuone, “Nenda kaonane nae, una nafasi ya kubadili historia ya mtoto huyo” alisema Emiliano.

Ronaldo hakuwa na mambo mengi akanyoosha mpaka alipo Mbappe, akamkumbatia kwa furaha sana, Mbappe hakuamini macho yake, na kwa vile ilikuwa majira ya baridi, Ronaldo aliwaomba walete sweta avae Mbappe, ndio lile sweta pichani akiwa na Ronaldo.

Mbappe alimuelezea mengi sana Ronaldo akiwa na miaka 13 tu, alimwambia kuhusu ndoto zake na namna anavyomuhusudu, Ronaldo tayari ni staa wa dunia ila amesimamisha muda kumsikiliza mtoto mdogo tu, baadae Ronaldo akaomba wapige picha, Mbappe alishasahau kuhusu picha.
Mbappe alimwambia Ronaldo siku moja atacheza nae Madrid, alimwambia siku moja atarithi kijiti chake, walimaliza mazungumzo na Ronaldo kuondoka zake, kuanzia siku hiyo Mbappe hakuwahi kurudi nyuma tena, Ronaldo alibadili maisha yake kabisa🙏 DREAM AND BECOME.
Naam, hapa ni mahali pako! Kuwa shujaa kwenye sloti hii ya Samurai Ken ujishindie mkwanja na kujipa burudani murua.



Hopemwaikuka
Waooo! Its so nice
Fatuma kasomo
Gud
Issa
Kylian mbape mtu makin sana
Amiri Kayera
Mbappe atakua tunu ya baadae
Elika
Mbappe Yuko vizur sana
Povel
Dream is can TRUE🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼
aisha
Mbappe mtu mbaya
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif
Venerose
Good
Angelina
Safi
Caroline
Mbappe ni fireee
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri mbappe kazana itawezekana akunakinacho shindikana
Mwajumah
Mbappe yupo vizuri sana
Mwanahamisi
Safi
Tatu
Mbappe awezi kukata tamaa hata kidogo
Adelta
Mpappe Yuko vizuri
jullie
aongeze juhudi tu
Saupha mohamed
Mbappe yupo vizur
Sauda
Mbappe anatisha
Sabrina
Atakua tu
Rehema
Good
magdalena
dogo umenena vyema na umeona mbali sana
Fatina mfigi
Mbappe namuona mbali hapo badae
zeiyana
hangoze juudi hanaweza hakawa zaidi ya Ronaldo kama hatajituma hipasavyo
Gabriel
Mbappe atakua tunu
warda
Dogo anakuja juu sana