Baada ya mechi kadhaa za mtoano za kombe la EFL kupigwa na washindi kupatikana ndani ha hatua itakayowezesha kila klabu kupata pacha yake ya kushindanishwa ili kuendelea kuchuja hadi kupata washindani wawili watakaokutana hatua ya fainali, tayari klabu kubwa zimeweza kushindanishwa katika hatua ya mwanzo kabisa ya kombe hilo.
Katika hatua hiyo, Chelsea watawakaribisha Manchester United huku wakikumbuka kipigo cha mapema sana kwenye ligi walichokipokea kutoka kwa vigogo hao, ambao walionekana kuwatawala wakati wa mchezo wao wa ligi hapo awali. Mbali na hilo, wawili hao bado wana la kufanya ili kujiimarisha zaidi kuweza kufanya vema kwenye mechi yao hiyo.
Huku wakubwa wengine wakikutana katika hatua hiyo hiyo ambapo Liverpool atamkaribisha Arsenal nyumbani kwake katika hatua hiyo ya mtoano ili kumpata mmoja pekee atakayefanikiwa kutoboa na kusonga mbele zaidi. Jambo ambalo linasubiriwa kwa shauku kubwa sana na kila mmoja kushuhudia soka safi kutoka kwa klabu hizo.
Chelsea ambao walifungwa goli 4 – 0 na United wameweza kupenya katika inayofuata baada ya kumwaga mvua ya magoli walipokuwa wakitafuta kusonga mbele huku wakiwachezeshea Grimsby Town kipigo cha 7 – 1, jambo ambalo linatazamiwa endapo ndiyo ubora wa kikosi hicho cha Lampard kwa sasa au kuna la zaidi kwao.
Wakati huo, wapinzani wao walipata ugumu kidogo baada ya kuweza kufika hadi hatua ya mikwaju ya penati ndani ya mechi yao na Rochdale baada ya mechi yao kuisha kwa sare ya 1 – 1, na United kufuzu kwa mikwaju ya penati ambayo iliweza kuwa 5 -3 na klabu hiyo ambayo ilionesha ukomavu wa aina yake.
Wakati vijana wa Klopp hawakuwa na ugumu wowote katika mechi yao baada ya kuwapa dozi Mk Dons magoli 2 – 0 ambapo kikosi cha Liverpool kiliweza kuwa na mabadiliko ya pekee sana ndani yake lakini hilo halikuweza kuwa na uzito wa aina yoyote kwa kikosi hicho ambacho kwao kupata matokeo mazuri imekuwa jadi yao. Huku mpinzani wake Arsenal akipata ushindi wa goli 5 – 0 dhidi ya Nottingham Forest.
Manchester City ambaye anashikilia taji hilo kwa msimu uliopita, atakutana na Southampton baada ya kuwaondoa Preston North End, wakati huo huo Everton wao wakiwekwa katika kapu moja la kucheza na Watford.
Mechi nyingine za hatua hiyo ni Aston Villa dhidi ya Wolves, Burton Albion na Leicester City, Crawley Town na Colchester United, na Oxford United dhidi ya Sunderland.
Kwa hatua hizo pekee basi washindi watapatikana ili kuumana kwa hatua nyingine tena.
Povel
Gud news