Man United Kutemana na Ed Woodward 2021.

Ulimwengu wa soka bado upo kwenye taharuki kufuatia kuzuka kwa mpango wa European Super League. Vilabu 6 vya EPL vimejiondoa katika hilo na Man United wataachana na Mkurugenzi wao mwishoni mwa 2021.

Mpango wa kuanzisha European Super League ulihusisha vilabu 12 barani Ulaya ambapo raisi ya Real Madrid – Florentino Perez angekuwa mwenyekiti wa mashindano hayo akisaidiwa na raisi ya Juventus – Andrea Agnelli na Joel Glazer (mwanafamilia ya wamiliki wa United)

Tangu kutangazwa kwa European Super League, wadau wa michezo duniani wamepinga vikali mpango huo kila mmoja kwa sababu zake. Uefa, Fifa, Serie A, LaLiga na EPL wameenda mbali zaidi wakitishia kuvifungia vilabu pamoja na wachezaji watakaoshiriki mashindano hayo.

Upande wa pili, licha ya Man United kuwa miongoni mwa vilabu vilivyohusika katika mchakato wa kuanzisha European Super League, klabu hiyo sambamba na Arsenal, Chelsea, Liverpool na Man City, vimejiondoa rasmi kwenye European Super League.

Ed Woodward akiwa Old Trafford.

Muda mfupi kabla ya United kujiondoa, klabu hiyo ilitoa taarifa kuhusu Mkurugenzi mkuu – Ed Woodward ambaye ni rasmi atajiuzulu nafasi hiyo mwishoni mwa 2021.

Ed Woodward alijiunga na United 2005 na kuisaidia timu hiyo katika nyakati mbalimbali kabla ya kuchukua nafasi ya David Gill kama mkurugenzi mkuu mwaka 2013.

Man United chini ya Ed Woodward imekuwa ikikosolewa kwa kushindwa kubeba taji la EPL sambamba na kutokuwa na sera nzuri ya usajili kwenye klabu hiyo. Wadau na mashabiki wengi wa United wamekuwa wakishinikiza Ed Woodward kuondolewa klabuni hapo kwa muda mrefu na pengine hii ikawa ni habari njema kwa wengi waliokuwa hawamuhitaji tena kiongozi huyo.

“Ninajisikia fahari kuitumikia United, ni heshima kubwa kuitumikia moja ya klabu kubwa duniani kwa takribani miaka 16. Klabu ipo katika muelekeo mzuri wa baadae na utakuwa ni wakati mgumu kuondoka mwishoni mwa mwaka huu.” alisema Ed Woodward.

“Kwa niaba ya kila mmoja Man United, ninamshukuru sana (Ed Woodward) kwa utendaji kazi wake na kujituma bila kuchoka. Mchango wake kwenye klabu ni mkubwa na ataendelea kukaribishwa Old Trafford kama mwanafamilia wa Man United alisema Joel Glazer.

Pengine huu utakuwa ni mwanzo mzuri wa United au tutegemee kitu gani pindi klabu hiyo itakapoanza maisha bila Ed Woodward?


MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

CHEZA HAPA

11 Komentara

    Haya mashindano yesha kuwa na mikosi tena

    Jibu

    Hapo mambo yashakuwa meusi

    Jibu

    Ss tunasubili kuona mwisho wake nn#meridianbett#

    Jibu

    Mhmh !

    Jibu

    Hili jambo sijui litakuwaje dhaa mambo magumu

    Jibu

    Kama United wameamua kweli watakuwa wamefanya Jambo la maana Sana sababu uyo alikuwa anaikwamisha Sana timu

    Jibu

    Dhuuuu

    Jibu

    Woodward anaikost united

    Jibu

    Mambo yamekuwa mabaya tena

    Jibu

    Dah

    Jibu

    Duuh sio poa

    Jibu

Acha ujumbe