Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer, amewashauri timu yake kuchukua saini ya Miralem Pjanic ili awe mrithi wa Pogba.
Ole ameyasema hayo baada ya tathmini ya muda kuhusu eneo lake la kiungo ambalo bado halijajua hatima ya Paul Pogba klabuni hapo, ambaye amebakiza mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia mashetani wekundu.
Kwa upande wa Pjanic, toka ujio wa Koeman amekuwa akipata wakati mgumu sana. Kuna uwezekano mkubwa sana wa mbosnia huyo kuondoka klabuni hapo majira yajayo ya joto.
Ole anaamini kuwa Pjanic anaweza kuja kucheza pamoja na Mc Tominay na kufanya makubwa kabisa kwa Manchester United. Ikumbukwe kuwa ripoti hii imetolewa endapo tu Paul Pogba ataondoka Man United.
Pogba ameeleza kwamba yupo katika kipindi cha furaha sana katika kikosi cha Man United na hakuna taarifa sahihi kama atasalia hapo au atatimka kwenda timu nyingine, ambapo Real Madrid na Juventus zimeonesha nia za kumpata.
Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.



Adelta
Miralem Pjanic naye yupo vizuri
[email protected]
Nashukuru kwa taarifa
warda
Asitupangie
Venerose
Kama anastahili wamsajil tu
aisha
Kama yuko vizuri wamsajili tuu
Magdalena
Duh Pogba hawezi kupata mrithi
Sarah
Wamsajili tu
Khadija
Kama yuko vizuli wamsajili
Lydia Emmanuel Magoti
Wamsajiri tuu
neema hassan
Asante kwa taarifa@meridianbettz
Saupha
Wamsajili