Kane Amshukuru Mourinho

Mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane amesema ilikuwa ni furaha kubwa kwake kufanya kazi na kocha Jose Mourinho.

Mourinho alitimuliwa kwenye timu hiyo baada ya kupata matokeo mabaya kwenye michezo yake sita mfululizo ya hivi karibuni. Kane kwa sasa ni kinara wa mabao kwenye timu hiyo amesema “Mourinho alikuwa mtu safi sana kwenye timu hiyo.

Kane

“Nakushukuru sana bosi kwa kila kitu, ilikuwa jambo zuri sana kuona kuwa tumefanya kazi pamoja.

Kwa hakika ulikuwa mtu muhimu kwetu, nakutakia kila la kheri kwenye majukumu yako yajayo” aliandika Kane.

Mourinho ametimuliwa siku chache kabla Spurs hawajacheza fainali ya Kombe la Carabao, dhidi ya Manchester City Jumapili ijayo na atalipwa pauni milioni 28, sawa na shilingi bilioni 69 za kitanzania.

Kane

Timu hiyo msimu huu imeshindwa kufanya mambo makubwa kwenye ligi ikiwa sasa inashika nafasi ya saba na pointi 50, imeshinda michezo 14 na kupoteza michezo kumi baada ya kucheza michezo 32.

Mbali na Kane, pia staa wa Spurs, Son Heung-min, amesema kuwa anamshukuru sana Mourinho kwa juhudi zote alizofanya kwenye timu hiyo.


MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

CHEZA HAPA

10 Komentara

    Shukurani ndio kila kitu

    Jibu

    Kane amefanya Jambo jema

    Jibu

    Wenyewe walikuwa wanapendana

    Jibu

    Ni Jambo jema kushukuru

    Jibu

    kane amefanya vizuri kwa kutoa shukurani

    Jibu

    Mourinho alikuwa na mchango mkubwa Sana ingawa haukuonekana

    Jibu

    Kane amefanya Jambo zuri

    Jibu

    Shukurani ndio kila kitu

    Jibu

    Vizuri sana

    Jibu

    Mourinho kocha mahiri

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.