Pambano la marudio kati ya mabondia waliochuana ulingoni mapema mwezi uliopita limeahirishwa kufuatia tishio la Virusi vya Corona. Pambano hili lilikuwa linatarajiwa kufanyia Julai 18 katika viunga vya Las Vegas.
Tyson Fury alimchapa bingwa ambaye hakuwahi kupoteza mchezo katika raundi 7 mwezi uliopita na kuchukua ubingwa wa WBC. Hii ilikuwa ni nafasi ya Wilder kutetea taji lake.
Kwa mujibu wa Promota Bob Arum ambaye anashughuka katika pambano hilo, akizungumza na ESPN, pambano hili limesogezwa mbele hadi mwezi Oktoba kwa sababu ya athari za virusi vya Corona kwenye ulimwengu wa michezo.
Arum amesisitiza kuwa mchezo wa ndondi sio mchezo wa pekee ambao unajitegema nje ya dunia, unahusika moja kwa moja na kila kitu kinachoendelea duniani hivyo hakukuwa na budi kufanya mipango mingine mpaka hali itakapokaa sawa.

