KLABU ya Simba Queens leo itapeperusha bendera ya Tanzania kuiwakilisha kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kanda ya Cecafa watakaposhuka leo saa 1 usiku kwenye uwanja wa Azam Complex kucheza dhidi ya She Corporate ya Uganda.

Hatua ya makundi ya michuano ya kuwania kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake ilikamilika wikiendi iliyopita huku ikishuhudia timu nne zikifuzu hatua ya nusu fainali, kila kundi kwa makundi yote mawili likitoa timu mbili ambazo ziliongoza.

Simba Queens walikua timu ya kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya kushinda michezo yao yote ya hatua ya makundi na kukusanya alama zote 9 huku timu ya She Corporate ya Uganda ambao wameshinda michezo miwili.

Walipoteza mmoja dhidi ya Simba Queens na kukusanya alama sita wakiungana na Simba kuendelea na nusu fainali kwa kutoka kudndi A.

Mabingwa wa ligi kuu wanawake nchini Ethiopia, CBE wameongoza kundi B kwa kushinda michezo yao yote ya hatua ya makundi huku timu ya As Kigali ya Rwanda wakiungana nao kwenye kipute cha hatua ya nusu fainali ambao walivuna alama sita.

Hatua hiyo ya makundi imeshuhudia timu 2 za mwisho kwenye kila kundi, yaani zilizoshika nafasi ya tatu na ya nne zikiaga mashindano kwa kutofuzu hatua hiyo ya mtoano kwani vigezo vilihitaji timu zitakazoshika nafasi mbili za juu kwenye kundi kucheza hatua ya nusu fainali.

Klabu ya Worriors Queens ya Zanzibar na Fofila PF ya Burundi kwa kundi B, Yei Joint Stars ya Sudan kusini na GRFC ya Djibouti ndizo zilizokosa vigezo hivyo vya kutoendelea na hatua za mtoano na kuaga mashindano

Kocha wa Simba Queens Sebastian Nkoma aliliambia Championi Jumatao kuwa: “Ushindi utapatikana na ninaona kabisa tunakwenda kucheza fainali. Msimu uliopita tulishindwa kutoboa lakini awamu hii tutakwenda.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa