Klabu ya Zamalek ya nchini Misri imrfanikiwa kubeba ubingwa wa ligi kuu nchini humo maarufu kama Egypt Premier League.

Zamalek wanafanikiwa kubeba ubingwa wa ligi kuu nchini humo ikiwa ni mara ya pili mfululizo baada ya kubeba ubingwa huo mwaka 2021 hivo inakua mara ya pili mfululizo kwa kutwaa ubingwa huo mwaka huu 2022.

zamalek, Zamalek Yatwaa Ubingwa wa Misri., Meridianbet

Zamalek wanabeba ubingwa wa Misri huku wakiwa wamebakiza michezo miwili mkononi na wanatawazwa mabingwa kwasababu hata wakipoteza michezo miwili iliobaki hawafikiwi kwa alama na anayeshika nafasi ya pili ambae ni klabu ya Pyramids yenye alama 68 huku klabu ya Zamalek ikiwa na jumla ya alama 76.

klabu ya Zamalek inabeba ubingwa huku mahasimu wao wakubwa klabu ya Al Ahly wakiwa wanachechemea huku wakiwa wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo. Zamalek sasa wanakua na jumla ya mataji 14 ya ligi kuu nchini humo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa