Tetesi zinasema, Borussia Dortmund wanataka kujaribu kumshawishi mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 21 kusalia klabuni humo.
Manchester City itasubiri hadi msimu wa joto ili kumsajili mshambuliaji, huku klabu hiyo ikiendelea kumtaka mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza Harry Kane na pia kuwa na Haaland miongoni mwa orodha ya walengwa.
Matumaini ya Barcelona kuongeza mkataba wa winga wa Ufaransa Ousmane Dembele yamepata pigo baada ya mazungumzo kuvunjika. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 unamalizika majira ya joto.

Newcastle United wanatumai kukamilisha dili la kumnunua beki wa kulia wa Atletico Madrid na England Kieran Trippier, 31, wiki ijayo na, baada ya kuumia kwa mshambuliaji wa Uingereza Callum Wilson, 29, pia watajaribu kusajili fowadi mwezi Januari.
Tetesi zinasema, Chelsea wameuliza kuhusu kupatikana kwa beki wa kushoto wa Ufaransa Theo Hernandez, 24, ambaye AC Milan haitafikiria kumuuza kwa chini ya euro 60m (£50.5m).
Meneja wa muda wa Manchester United, Ralf Rangnick amemwambia mlinda mlango wa Uingereza Dean Henderson kwamba hataruhusiwa kuondoka katika klabu hiyo mwezi Januari.
Tetesi zinasema, Kipa wa Tottenham Hugo Lloris, 35, yuko tayari kurejea katika klabu yake ya zamani ya Nice wakati mkataba wake na klabu hiyo ya London utakapokamilika msimu wa joto.

Sevilla hawana nafasi ya kuongeza ofa yao kwa mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial baada ya Manchester United kukataa hatua ya klabu hiyo ya Uhispania kumchukua kwa mkopo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.
Tetesi zinasema, Besiktas wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Uturuki Cenk Tosun kutoka Everton kwa mkopo.
Juventus watakuwa tayari kumuuza winga, Dejan Kulusevski mwenye umri wa miaka 21 kwa euro 35-40m (£29m-34m) mwezi Januari, huku Arsenal, Tottenham na Bayern Munich wakiwa washindani wakuu.
Unaanzaje siku yako katika msimu huu wa sikukuu, mchongo upo meridianbet kasino. Sloti pendwa ya Sahara Richies inaweza kukufanya ukawa milionea katika kufunga mwaka huu, Jiunge na ufurahie kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa.

CHEZA HAPA

