UEFA: Bayern vs PSG ni Mechi ya Kipekee

Fainali ya Ligi ya Mabingwa – UEFA kuhitimisha msimu wa 2019/20. Ni mtanange wa aina yake utakaowakutanisha miamba ya Ujerumani – Bayern Munich dhidi ya matajiri wa Paris – PSG.

Kiufundi, huu ni mchezo ambao utakuwa wa aina yake. Timu zote 2 zina nafasi ya kumuumiza mwenzake na kuandika historia ya namna yake. PSG wamefika Fainali ya UEFA kwa mara ya kwanza na wanatazamia kubeba kombe hilo kwa mara ya kwanza katika historia ya timu hiyo.

Bayern Munich sio wageni wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa, lakini wanataka kuweka rekodi ya kubeba makombe 3 kwa msimu mmoja wakiwa tayari wameshabeba mawili kunako Bundesliga.

Upekee wa Fainali ya UEFA upo kwenye mifumo ya uchezaji wa timu hizi.

Bayern wamekuwa wakitumia sana mfumo wa 4-2-3-1, mfumo ambao umelenga zaidi kushambulia na unawatumia mabeki wake wa pembeni katika kushambulia. Huu ni mfumo ambao umewapatia matokeo mazuri wakiwa hawajapoteza mchezo wowote katika mechi 29.

uefa

Mfumo huu ndio uliopeleka vilio Barcelona na Lyon. Hawapotezi nafasi kirahisi na kuwapa shida wapinzani. Uwezo wa wachezaji mmoja mmoja katika kikosi cha Bayern pia ni faida katika mfumo huu. Gnabry, Alphonso Davies, Kimmich, Lewandowski,Muller na Perisic ni kati ya wachezaji muhimu wa Bayern.

Pamoja na ubabe wa Bayern, kama watajisahau sehemu yeyote, Mbappe, Di Maria na Neymar watawaumiza kutokana na uwezo wao wa kukimbia na mipira.

Kwa upande wa PSG, wao wanatumia zaidi mfumo wa 4-3-3 pamoja na uwezo binafsi wa wachezaji wao hasa washambuliaji. Uwezo wa Mbappe akiwa na mpira na kasi aliyonayo ni dhahiri mabeki wa Bayern watakuwa na kazi ya ziada.

Neymar amekuwa akichezewa faulo nyingi kutokana na namna ya uchezaji wake unaotumia ujuzi mwingi na mbio. Kwa namna ya uchezaji wake, timu pinzani nyingi zinakuwa na wakati mgumu kumkaba kwani nafasi ya kupata kadi ya njano au nyekundu ni kubwa.

Di Maria amekuwa akisahaulika mara kadhaa na mabeki wa timu pinzani, lakini mashambulizi ya PSG yanachochewa na uwezo wa winga huyu mwenye spidi na ufundi wa kutumia mipira ya adhabu.

Kwa sababu hizi na nyingine nyingi, ni dhahiri kumtaja bingwa wa mchezo huu ni ngumu lakini ni mchezo utakuaokuwa na magoli kwa timu zote endapo kila timu itatengeneza na kutumia nafasi za magoli.


Drops and Wins!

Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.

Soma zaidi Ucheze

43 Komentara

    Ukiangalia vikosi vyote viwili unapata picha ya soka tamu sana na magoli ya kideo siku ya fainali, sio mechi ya kukosa kuangalia

    Jibu

    Tutaona ufundi mwingi kwenye hii mechi lakini mwisho wa siku bayern atabaki na ndoo tu haina ubishi

    Jibu

    Kwelii mechii sio za kitoto hizoo.

    Jibu

    Mapema kitaeleweka

    Jibu

    Bora kieleweke

    Jibu

    Kwa kuangalia hii gemu hunaona kabic Bayern kesho hawana kazi ngumu kabic ila tusubiri tu kuwapa pongezi PSG kwa kushiriki na sio kua mabingwa si kweli

    Jibu

    Hatarii hii

    Jibu

    Mtanange mkali sana

    Jibu

    Huu mchezo autaji hasira kila kikosi Leo kimejipanga sawasawa PSG atoweza kumuachia bayern

    Jibu

    Mechi kali sana

    Jibu

    Mechi sio ya kukosa kabisa nataka niwaone watoto wa matajiri PSG watakavyo fanya yao

    Jibu

    Nimewakataa sana Bayern kwa muda ila katika fainali naimani atamfunga PSG na kunyakua taji ingawa itakua mechi ngumu sana ya kukata na mundu si ya kukosa kuiangalia

    Jibu

    Kweli mechi hizi sio za kitoto#Meridianbettz

    Jibu

    kabisa ni mechi ya kipekee inayosubiriwa kwa hamu kubwa na tulio wengi

    Jibu

    Hatari hii#meridianbettz

    Jibu

    Hatarii bonge lamechi apatoshi hio mtanange nyavu kutikiswa kila goli lamtu lazima kushambuliwa

    Jibu

    Hii mechi Kali sana tunasubiri kwa hamu tuone matokeo@meridianbettz

    Jibu

    Huu mtanange mzito Kila timu ipo vizur ukiangalia bayern wapo vizur psg nao wamoto kwaiy hii mechi itakuwa nzur San Ila wenyew wanakwambia mpira dakika 90 ngoj tuone!!

    Jibu

    Tunasubiri fainali kwa hamu

    Jibu

    Hii mechi Kali sana tunasubiri kwa hamu tuone matokeo @meridianbettz

    Jibu

    Vikosi vyote bola

    Jibu

    Mambo mazur

    Jibu

    Tunasubili kuiona fainali kwa hamu sana maana patakua hapatoshi

    Jibu

    Wabashiri kote duniani tunaipa nafasi Bayern lakini ktk mchezo lolote linaweza kutokea kwa anayeamuka vizuri hushinda na anayeamuka vibaya hupoteza. Pamoja na ufundi wa kocha lakini wakati fulani ni bahati ndi huchukua nafasi zaidi#meridianbettz

    Jibu

    Hii mechi ni balaa maana wote wako vzur

    Jibu

    Don’t miss

    Jibu

    Safi

    Jibu

    bayern piga hao kama kawa ida yetu LIKE FATHER LIKE SON baba kafa 8 bado mtoto

    Jibu

    Hii mech n ngumu sana na kutokana na mifumo yao ya uchezaji wote n wa ushambuliaji hapa ninamaana mechi itakuwa ya kibabe balaa

    Jibu

    Hii mechi itakua inamagoli mengi maana kila timu naona safu ya ushambuliaji iko vizuri kuzidi safu ya ulinzi

    Jibu

    Nyasi zitawaka moto sio kwa kandanda iloooo!!!

    Jibu

    Hii fainali ni ya mvuto Sana maana inawakutanisha mabingwa wa ligi mbili tofauti.

    Jibu

    Vikosi vyote viko vizuri

    Jibu

    Hii hatumwi mtu dukan

    Jibu

    Kwa upande wa PSG, wao wanatumia zaidi mfumo wa 4-3-3 pamoja na uwezo binafsi wa wachezaji wao hasa washambuliaji. Uwezo wa Mbappe akiwa na mpira na kasi aliyonayo ni dhahiri mabeki wa Bayern watakuwa na kazi ya ziada.

    Jibu

    Kabisa Ni mechi ya kibabe

    Jibu

    Safu zote ziko vizuri pamoja na wachezaji wao hapa haifahamiki nani ataondoka na ubigwa huo mana wrote wanauwezo Wa juu sana hivyo tunasubiri kuona dk 90

    Jibu

    Hakika mtanange mkali Sana patakuwa hapatoshi

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Utakua mchezo wa kusisimua.

    Jibu

    Itakua balaa

    Jibu

    Itakua hatari.

    Jibu

    Kwa kweli ilikuwa Ya kipekee#Meridianbettz

    Jibu

Acha ujumbe