Ukweli haujui uongo ila uongo siku zote unaujua ukweli, ili uwe mkweli unahitaji tu kuwa mkweli, lakini ili uwe muongo lazima uishi katika kivuli cha ukweli siku zote. Ibrahimovic amechagua kuishi katika kivuli cha ukweli, moyo wake uliojaa uongo umeulevya mpaka ubongo wake, kikombe cha mahaba juu ya kipaji chake kimemfanya kuwa mtumwa wa nafsi yake.

Nafsi yake haishi tena ile kweli anayopaswa kuishi, inamfanya kujiona ndiye mchezaji bora kuwahi kutokea duniani, ameamua kuwa kinyume na dunia nzima ya soka. Kibaya anaona dunia ndiyo inamkosea heshima sana, heshima wanazopewa Lionel messi na Cristiano yeye alistahili kupewa zaidi yao, hatazami makubwa waliyofanya.
Akiwa Barcelona Zlatan Ibrahimovic aliwaita Messi, Iniesta na Xavi kuwa ni watoto wa shule wanaopendelewa na mwalimu wao, kipindi hicho akiwa ni Pep Guardiola, hakuona sababu ya wao kuonekana bora wakati yeye akiwepo.

Kwa Zlatan anaanza Zlatan ndo wengine wanafuata, Pep Guardiola hakulijua hili mpaka alipoambiwa huwezi kumuweka nje mungu wa mpira kwa ajili tu ya genius messi. Akaondoka zake Nou Camp, moyoni akiamini Lionel Messi hakustahili kuonekana bora zaidi yake ila akilini akauficha uwezo wa kufunga wa Lionel Messi.
Kwa Cristiano Ronaldo, Zlatan Ibrahimovic atakwambia Ronaldo anayemjua yeye vizuri ni yule Ronaldo de lima wa Brazil, hamfahamu mwingine, inawezekana ikawa sahihi kwake. Lakini uongo siku zote unatafuta njia zake kuficha ukweli, atakwambia tena huyu wa sasa ni zao la mazoezi tu kipaji cha mpira hana, kumbe anamjua Cristiano Ronaldo ni ngumu kuuficha ukweli.
Mazoezi ya mpira ni chakula cha kila mchezaji, mbona wanazidiana ubora sasa, anatuthibitishia maneno ya kuwa uongo una njia fupi. Kwa Zlatan Ibrahimovic pia anamuona Pele kama mtu aliyebebwa na nyakati, kwake hana maajabu yoyote yale, amenda mbali na kusema kama yeye angezaliwa enzi za kina Pele zilizokua hazina VAR angeweza kufunga zaidi ya goli 3000.


Mwanaidi
Hata iweje hawezi kuwafikia hao watu labda wastaafu mpira ndio aweze kusema hivo
Evaluziga
Hana jeuri ya kuwafikia hao labda wastaafu ndio aseme ivo
Devotha
Zlatan ukubali ukatae Ronaldo bado yupo juu sana kwako
Adelta
Ronald Yuko vizuri sana
Hana mpinzani
Agness
Ronald ni bonge la mchezaji
Rehema Dickson
Ni mtazamo wake kama anaona yy ni bora kuliko wao sawa yuko sahihi sio mbaya kujiona bora sifa jipe kwanza mwenyewe na ndo utasifiwa na watu wengine
Khadija
Ronald yupo vzr sana#meridianbettz
Hope mwaikuka
Ni mtazamo wake so m n nan mpaka nipinge
Antony Luseno
Uwo ni mtazamo wake labda kutokana amecheza timu kubwa zote za ulaya
Ester jackson
Huu ni ujasiri wake tu ukweli tunaujua sisi mashabiki ila kwake ni Sawa kabisa haha ha ha
Frank Patrick
Zlatan kacheza team kubwa nyingi Ulaya ila kaziletea mafanikio gani?labda bora kwa kalate
Neema juma
Ronaldo atabaki kuwa Ronaldo mkali wao
felister
Ayo ni mawazo yake lkn Ibrahimovick yeye sio Bora kuliko Ronald km ni ivy mbn hana ata tuzo moja
Ester mmakasa
Zlatan Ibrahimovic atasubiri sana kwa hao wamba wawili..
winfrida
kweli ni mchezaji mzuri lakini umfikii ronaldo na messi
Emmy cleopa
Ronaldo yuko vizur sana
Theckla
Ronaldo hana mpinzani
Tahiya
Huo ni mtazamo wke tyuu tena wa kichuki kabsa uwezi jiona bora kwa wenzio ikiwa wanaokuona ukicheza hawaoni ubora wako Zlatan ni mzuri ila kiwango chake sio sawa na Ronald na Messi
Hamidu
Messi & Ronaldo wachezaji wa sayari nyingine#
Ernest
Kuna vitu vichache tuu Kadabra amevikosa na kumfanya azidiwe na Messi na Ronaldo lakini kiukweli huyu jamaa ni hatari sana
Sadick
Jamaa ana majidai mengi sana, siku zote anajiona bora kuliko wote. Hata hivyo ni mchezaji mzuri#meridianbettz
Samiah
Ronaldo mtu mmbaya sanaaa
Genia Sikaluzwe
Ronaldn ni mchezaji mzuri
Tatu
Rinaldo na Messi ni wachezaji hatari sana mtu yoyote asijifananishe na watu hao
mathayo sonje
Ingekua bongo tungesema anatafuta kiki, lakini yeye huko aliko anatafuta nini? anajua fika hiki ni kipindi cha ronaldo na mess!!! naona amesahaulika anataka kukumbusha watu kua na yeye yupo.
Salma
Kila 1 ana mtazamo wake na jinsi anavyojiamini
mwakalosi
labda bora wa taekwando mpira atuache tu
Zeiyana
Kila mtu hanajivunia alicho nacho messi anauchezaji wake lonaldo hanauchezaji wake na yeye anajivunia alichokua nacho
Lydia Emmanuel Magoti
Nimtazamo wake labda amecheza timu kubwa zote za ulaya
Swai
Akiwa Barcelona Zlatan Ibrahimovic aliwaita Messi, Iniesta na Xavi kuwa ni watoto wa shule wanaopendelewa na mwalimu wao, kipindi hicho akiwa ni Pep Guardiola, hakuona sababu ya wao kuonekana bora wakati yeye akiwepo.#meridian
Caroline
Ibrahimovic hampati ronaldo
Lombo
aache ndoto zake za mchana labda ajilinganishe na MESS na sio CR7 zile levo nyingne
Povel
Ni Bora Ila hawez kuwah Bora kuwazid Messi na Ronaldo thnks meridian bet tz kwa update
Shafii
Ni mtazamo wake yeye
Kenani
Hakuna kitu kivuzr kwenye mapambano Kam kujiamin silaha ya Kwanza kweny kupambana ni kujiamin
Aziza mushi
Ila messi na Ronaldo wanauwezo Sana.
David pere
Kwa maoni yake na anvyojikubali mwenyewe Ndio maana anasema hivyo
Warda
Zlatan Ibrahimovic huwaga sio shabiki yangu kabisa #Meridianbettz
Gabriel
Yupo sahihi kwa upande wake