BODI ya ligi kuu (TPBL) limeihamisha timu ya Kagera Sugar Jijini Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba baada ya uwanja wao kuwa na mapungufu.
Kagera imeutumia uwanja wao wa Kaitaba leo kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Big Stars.

Barua kutoka TPBL iliyotolewa leo imeeleza kuwa timu hiyo itautumia uwanja wa CCM Kirumba uliopo Mwanza kutokana na marekebisho mbalimbali kutokamilika.
Marekebisho hayo ni kutokuwepo kwa uzio wa kutenganisha mashabiki na eneo la kucheza hivyo kuhatarisha usalama wa wachezaji.
Kamati ya leseni za klabu itaruhusu uwanja huo kutumika baada ya kuukagua na kujiridhisha kuwa mapungufu hayo yamerekebishwa.

