Hatimaye mwamuzi wa mchezo wa ligi kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Simba ametangazwa rasmi leo ambaye ni Ramadhan Kayoko.
Mchezo huo wa Dabi ya kariakoo utapigwa jumapili saa 11:00 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam huku mchezo ukitarajiwa kusimamisha nchi kwa dakika 90 ili kushuhudia mtanange.
Mwamuzi wa kati wa mchezo huo ni Ramadhan Kayoko akisaidiwa na Mohamed Mkono na Janeth Balama huku mwamuzi wa akiba ni Elly Sasii.
Pia Mgeni rasmi katika mchezo huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa.

