BAADA ya kuondoka kwa Walter Harrison, Uongozi wa klabu ya KMC umemtangaza Daniel Mwakasungula kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo.

Walter ambaye aliiongoza klabu hiyo kwa mafanikio makubwa aliondoka hivi karibuni kwenye klabu hiyo na kujiunga na klabu ya Yanga.

YANGA, KMC Yamtangaza Mrithi wa Meneja Yanga, Meridianbet

Majukumu aliyonayo Walter ndani ya klabu ya Yanga kwa sasa ni kuwa Meneja wa kikosi hicho ambacho jumamosi kilitwaa Ngao ya jamii baada ya kuifunga Simba kwa mabao 2-1.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka KMC zimeeleza kuwa “Bodi ya klabu ya KMC imemteua Ndugu, Daniel Mwakasungula kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu”. 

Kikosi cha KMC kinatarajia kushuka dimbani Agosti 17, mwaka huu kumenyana na Coastal Union kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa