Ni ngumu kutazama mwisho wa jambo kuliko mwanzo wa jambo, mwisho wa jambo siku zote hubeba kumbukumbu zisizofutika baina ya pande mbili, haswa zikiwa ni kumbukumbu zilizojaa upendo unaoishi moyoni.
Kumbukumbu kumhusu kiungo James Kotei bado zinaishi ndani ya wanasimba, zimegoma kufutika kirahisi haswa wakitazama mwisho wao ulivyokuwa mzuri. Mwisho wa James Kotei ndani ya Simba ulijaa machozi yenye furaha ndani yake, hakuna aliyetamani yaishe, kila shabiki alitamani kufunga mlango wa Kotei kuondoka Tanzania.

Simba yenye miguu ya James Kotei ilikua salama salimini, alijua namna kiungo wa kati anatakiwa kuwa, pindi timu ikiwa haina mpira, ubongo wake ulisoma movement za wapinzani na miguu yake ikapokea maelekezo sahihi ya kupokonya mpira vyema.
Sura ya tabasamu ya Jonas Mkude pale katikati ya uwanja sababu yake kubwa ilikua katika miguu ya James Kotei, maana alimhakikishia pasi pindi atapohitaji kuzipeleka mbele na muhimu zaidi usalama wa timu pindi atapopanda juu kupiga mashuti. Mwalimu Patrick Aussems alikua na uhakika na kile alichokuwa anakifanya sana James Kotei hadi akafikia kuwaruhusu wakina Emmanuel Okwi kuwa free muda wote kuchezea mpira, ni miguu ya Kotei iliyofanyika kafara ili tu timu icheze vyema.
Viungo wa timu pinzani walimchukia pale alipokuwa anakaba, lakini walimpenda pale walipokuwa wanampiga rafu, alikua ananyanyuka taratibu anafurahi, ilikua ni nadra sana kuiona sura ya Kotei ikiwa na hasira.
Akitoka nje ya uwanja anavaa jezi ya taifa stars anapiga selfie, tunamuona ni mmoja wetu, alijua kutufurahisha na tukafurahi kumuona akifurahi. Katikati ya furaha ghalfa James Kotei akatangaza kujiunga na Kaizer Chief, iliwastua wengi sana, ni ngumu sana kupokea mkono wa kwaheri katikati ya furaha ni ngumu sana.

Ingawa machozi yanawahi kukauka lakini macho siku zote hubaki kuwa na majonzi bado majonzi ya kumbukumbu ya James Kotei yanaishi katikati ya wanasimba. Ukitaja jina lake picha inayokuja ni kiungo aliyejua nini Simba inataka katikati ya uwanja, atabakia kukumbukwa kwa sababu kwa heri yake alitoa katika ya upendo na furaha, atabaki James Kotei atabaki James mwana wa Kotei.


Neema hassan
James kotei alikuwa na mchango mkubwa katika game
Mwanaidi
Lazima akumbukwe kotei alikuwa kiungo muhimu sana kwenye klabu
Elika
Hakika wekundu wa msimbazi bado tunamkumbuka sana james.hatutaweza kumsahau kamwe
Devotha
Poleni sana wanasimba kwa kubaki na kumbukumbu
Salma
Kumbe aliwapa kumbukumbu nzuri wana simba
Ester jackson
Simba walijawa machozi yenye furaha ndani yake, hakuna aliyetamani yaishe, kila shabiki alitamani kufunga mlango wa Kotei kuondoka Tanzania tunamkumbuka sana shujaa wa simba
Agness
Lazima akumbukwe alikua mchezaji mzuri Sana
Neema juma
Upendo mkubwa na kujituma kwake kutawafanya wana simba kutokumsahau kirahisii.JAMES KOTEI atabaki james mwana wa kotei jembeee
Rehema
James aliwapa kumbukumbu mzuri sn kwenye gemu
Samiah
Jemes aliwapa kumbukumbu
Rehema Dickson
hakuna aliyetamani yaishe, kila shabiki alitamani kufunga mlango wa Kotei kuondoka Tanzania tunamkumbuka sana shujaa wa simba
Hope mwaikuka
Alkua vizur sana enz hzo
Antony Luseno
Kotei ni mchezaji mahiri sana na simba hawakukosea kumsajili
aisha
James koteo yuko vizuri namkubali sana
Frank Patrick
Kaizer Chief ni club kubwa sana tumtakie kheri kwenye changamoto yake hiyo mpya ya kisoka
felister
James Kotei atakumbukwa daima
Ester mmakasa
James kotei ni kumbukumbu kwa sababu alifanya vizuri sana na alikuwa ndo kila kitu msimbazi ,anafaa kuigwa na wachezaji wengine wa timu mbalimbali.
Tahiya
James Kotei ukitaja jina lake picha inayokuja ni kiungo wenye kujua nini afanye katikat ya uwanja hakika wana simba tulijivunia nyakay ulizokiwepo simba
Hamidu
Mmoja wa kiungo Bora wakabaji
Waliocheza Simba sc kwa mafanikio#meridianbettz
Emmy cleopa
Ahsante kwa habari
Isaya massawe
Kafanya vizur sana pale simba
Ernest
Kotei anajuwa sanaaa
Sadick
James Kotei bado ana nafasi kucheza tena Simba#meridianbettz
Asia Abdy
Makala nzur. Meridian
dorophina
Kotei anajua sana
Furahav
Hii habari imenifurahisha sana,sababu umeniletea mchezaji ambaye nampenda sana mana anakaba hadi kivuli.
Mwanahamisi
James kotei Yuko vizuri
Tatu
Simba awatasahau hii kitu
Lydia Emmanuel Magoti
Kotei alikuwa mchezaji mzuri Sana kwenye krabu yamsimbasi kwai hawata msau nawatazi kumzungumzia mchezaji huyo anajua James kotei
Zeiyana
James kotei bado tunamkumbuka wana simba
Swai
Kumbukumbu kumhusu kiungo James Kotei bado zinaishi ndani ya wanasimba, zimegoma kufutika kirahisi haswa wakitazama mwisho wao ulivyokuwa mzuri #meridian
Genia Sikaluzwe
James kotei yuko vizuri Sana
Caroline
James Kotei we miss u
Mwajuma
Nimchezaji mzuri aliecheza simba kwa mafanikio
Lombo
zilipendwa
Povel
Ni mmoja Kati ya kiungo Bora wa kimataifa kuwah kutokeah mitaaa ya msimbazi thnks meridian kwa update
Kenani
Simba walipata mtu ambae ewasaidia sana
Shafii
Jamaa fundi
David pere
Kotei mtu hatari sana Yani sijui kwanini Simba wamemwachia aondoke
Warda
Kotei mnyama #Meridianbettz
Magdalena
Kotei alikuwa kinara mzuri alokubalika kwa kila mtu
Mariam mtandama
Alikuwa mzur