Haaland Afananishwa na Messi na Ronaldo.

Erling Haaland amekuwa na kiwango sawa akiwa na umri mdogo kama ilivyokuwa kwa Lionel Messi na Christiano Ronaldo, hii ni kwa mujibu wa kocha wa Norway Lars Largeback.

Haaland mwenye umri wa miaka 20 alikuwa na msimu mzuri 2019-20 akiwa na timu ya Borussia Dortimund baada ya kusajiliwa akitokea klabu ya Salzburg mwezi Januari.

Mchezaji huyo mtaifa wa Norway alifunga jumla ya magoli 28 katika michezo 22 akiwa na Slzburg katika mashindano yote, kabla hajaongeza mengine 16 katika michezo 18 akiwa na BVB.

Dortimund wameshindwa kutwaa taji la Bundesliga tangu mwaka 2011-12 na kuwaacha Bayern Munich waendelee kutawala, lakini Haaland ameleta matumaini kwa msimu unaokuja kama Dortimund wataendelea kuwa na mshambuliaji huyo.

Mshambuliaji Erling Haaland

Haaland alihusika kwenye magoli wakati Norway ilipo iburuza Austria kwa 2-1 na kumfanya kocha Largeback aamini umuhimu na ubora alionao mchezaji Haaland.

“Huenda nimekaa muda mrefu sana sijamuona mchezaji mzuri kama huyu tangu nishuhudie kwa Messi au Ronaldo kipindi wapo kwenye umri mdogo kama Haaland,” Largeback aliongea hayo kuelekea mchezo dhidi ya North Ireland katika mashindano ya Nations League.

“Kama hatoandamwa na majeraha basi tunaweza kusema kwamba kijana atakuwa mchezaji wa hadhi ya dunia kutokana na kiwango na ubora anaoonesha.”


SHINDA NA HI LO

Sasa hii ni rahisi zaidi kupata USHINDI! Unatabiri karata ipi ipo chini au juu, kisha unakusanya mkwanja wako.

Cheza sasa

39 Komentara

    Mmh kwa upande wangu hapa mess na Ronaldo ni miamba mingine ile aifananishwi asee

    Jibu

    Bado hajafika kiwango cha kuwafikia messi na Ronaldo.

    Jibu

    Kama hatoandamwa na majeraha basi tunaweza kusema kwamba kijana atakuwa mchezaji wa hadhi ya dunia kutokana na kiwango na ubora anaoonesha.

    Jibu

    Atakuwa bado hajafikiwa kiwango Cha Messi na Ronaldo.

    Jibu

    haongeze bidii tu anaweza fikia lekodi ya mahasimu hao

    Jibu

    Sidhani kama atapata iyo nafasi ya kufikia kiwango hiko

    Jibu

    Bado ajafika kiwango cha messi na ronaldo

    Jibu

    Halaand amekuwah kwny ubora sana kipind hch katika umri wake mdg natumai mbelen hatakuw na ubora wa messi$ Ronaldo hila kwa kipind hch ni vigumu kumeongeah maneno mengi kuhus yy kwn viwa go vya wachezaj vimekuwah vya kupanda na kushuk ila natumai anawezafik ubora wa magwij hao wa soka

    Jibu

    Messi na Ronald Ni watu hatari@meridianbettz

    Jibu

    Uenda akafikia viwango vya akina messi na cr7 ni swala la muda

    Jibu

    Erling Haaland ndiye mrithi sahihi wa CR7 kutokana na aina ya uchezaji wake hili halina ubishi

    Jibu

    kila kitu ni malengo akijitahidi atakua kama messi na Ronald hakuna kinachoshindikana

    Jibu

    Haaland ni fowad ambae akiwa kwenye kumi na nane akuachi hilo amedhihirisha mechi kumi za mwanzo akiwa na dortmund

    Jibu

    kuwafikia hawa vinara ni kazi kubwa sana inayohitaji juhudi za kutosha uenda akawafikia

    Jibu

    Bado hajafikia kiwango cha messi wala Ronaldo kama hataongeza jitiada haweza kuwafikia ila hapambane sana

    Jibu

    Mmmm bado kabisa sijaona majabu yake kuwafiki hao watu

    Jibu

    Endapo msimu Erling Haaland atakuwa moja ya top scorers wa Bundesliga saini yake itawaniwa na kila timu kubwa na bei yake itakuwa kubwa ya kutisha#meridianbettz

    Jibu

    Ha aah wapi bado hajafikia hapo ajitahidi atafika tu

    Jibu

    Haaland anauchezaji fulani ivi ameizing na ndio maana anafananishwa na messi na Ronaldo

    Jibu

    Hakuna kitu kama hicho#meridianbettz

    Jibu

    Haaland kama anataka kufika kiwango cha mess na Ronaldo itambidi aongeze juhudi kwenye kiwango chake cha kucheza na ajitume sana

    Jibu

    Mmh bado hajafikia kiwango Cha Messi na Ronaldo#Meridianbettz

    Jibu

    Apambane sana kufikia level za kina Messi na Cr7

    Jibu

    duuh

    Jibu

    Yuko vizuri ila bado hajafikia hizo hatua za kufananishwa na messi na Ronald.

    Jibu

    Bado sanaaa

    Jibu

    Bado hajafikia kiwango

    Jibu

    Umakini wake kwenye kumi nane utamfanya afikie viwango hivyo

    Jibu

    Kwasasa wanamtwish mzg kufananish na hao watu

    Jibu

    Bado sana

    Jibu

    Halaand amekuwah kwny ubora sana kipind hch katika umri wake mdg

    Jibu

    Duuuh!

    Jibu

    Khaaa

    Jibu

    Bado hajawafikia

    Jibu

    Akaze sana sio kirahisi rahisi hivyooo!!

    Jibu

    Bado aongeze juhudi

    Jibu

    Aongeze juhudi

    Jibu

    Mmh kwa upande wangu hapa mess na Ronaldo ni miamba mingine ile aifananishwi asee

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.