BONDIA maarufu Bongo, Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ ameondolewa kuzipiga na bondia kutoka DR Congo Alex Kabangu na nafasi yake imechukuliwa na Hussein Itaba.
Pambano hilo limepangwa kufanyika Novemba 13 ukumbi wa Next Door Arena, Oysterbay na siku hiyo pia bondia nyota nchini Hassan Mwakinyo atapigana na bondia Jose Carlos Paz kutoka Argentina akiwania mikanda miwili.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni Jackson Sport, Kelvin Twissa amesema kuwa mabadiliko hayo ni kawaida kutokea katika masuala ya ngumi za kulipwa bondia huyo (Itaba) ameanza mazoezi kwa ajili ya kupambana na Kabangu.

Hivi karibuni, Mbabe alipigwa kwa pointi dhidi ya bondia Bek Nurmaganbet mjini Atyrau, Kazakhstan. Bondia huyo alikwenda kupigana chini ya promota Juma Msangi maarufu kama Jay Msangi.

“Tumeona tufanye mabadiliko katika moja ya pambano letu kwa lengo la kupanua wigo na kujenga heshima katika ngumi za kulipwa nchini, hivyo mabadiliko hayo yamefanywa ili kupanua wigo wa mabondia na kuinua vipaji zaidi hapa nchini, naamini Itaba atafanya vyema katika pambano hilo,” alisema Twissa.
Amesema kuwa maandalizi ya mapambano ya ‘Dar Fight Night’ yanaendelea vizuri huku bondia bingwa wa mabara wa uzito wa superwelter Hassan Mwakinyo akijifua vikali.
Mbali ya kutetea mkanda huo, Mwakinyo pia atawania ubingwa wa mabara wa uzito huo huo wa Chama cha IBA.
Mabondia kutoka nchi tano watazichapa kumsindikiza Mwakinyo na Pazi, akiwamo aliyekuwa bingwa wa dunia wa WBC, Fatuma Zarika kutoka Kenya. Zarika atazichapa na Patience Mastara wa Zimbabwe, na Zulfa Yusuph Macho atacheza na Alice Mbewe wa Zimbabwe.
Amesema kuwa wameamua kuingia kwenye mchezo wa ngumi kutokana na kutambua vipaji vya mabondia mbalimbali hasa Mwakinyo ambaye anafanya vizuri katika mapambano yake.
“Siku hiyo kutakuwa na mapambano makubwa ambapo mabondia kutoka nchi sita, Argentina, DR Congo, Kenya, Zimbabwe na wenyeji Tanzania watapigana, ni siku ambayo mashabiki wa ngumi za kulipwa wataona kitu tofauti kabisa katika mchezo huo, “amesema Twisa.
Amesema kuwa kampuni yao chini ya udhamini wa Azam TV, colosseum hotel Dar es salaam na Asas ina uzoefu mkubwa katika kuandaa matamasha, masoko na shughuli mbalimbali na kuahidi kufanya jambo la kihistoria hapa nchini.
Hii ni halisi kwa ajili ya mashujaa wote! Ukiwa jasiri unavuna mkwanja kibao hapa na sloti hii ya Huangdi Casino. Waka nusu tukupe maradufu!



Dorophina
Dulla mbabe angekutaka na Alex ingekuwa poa sana
Ester jackson
Kwanini ametolewa kwenye mapambano Dulla Mbabe
Caroline
Dahh pole Sana Dulla
Tatu
Pambano litakuwa languvu
Sauda
Itaba ngumi jiwe.
Sabrina
Duuh Dilla mbabe yamemkuta yepi!
Mwajumah
Pambano la kukata na shoka
Fatina mfingi
Pambano kali
zeiyana
me naona ni vizuri walivyomtoa dulla mbabe hii itakua nafasi yake ya kumpunzika na kujenga afya yake vizuri
Povel
Masubwi mambo ni moto huko
warda
Ila Dull anapigana jamani