Uchambuzi: Brentford vs Newcastle United.

Steve Bruce anahofia kuhusu mchezaji wa zamani wa Newcastle ambaye amekuwa tishio, Ivan Toney ataleta tabu pale timu yake itakapo safiri kwenda Brentford usiku wa leo.

Uchambuzi: Brentford vs Newcastle United.

Alijiunga na Brentford kwa pauni milioni 5 mwezi Septemba, amekiwasha ndani ya michuano ya Championship akiwa na mabao 16 msimu huu.

Na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 sasa anatafuta kuvuruga ndoto za timu yake ya zamani kwenye michuano ya Carabao Cup kwa kuwakimbiza kwenye nusu fainali.

Bruce alisema: “Amefanya vizuri sana. Inaonekana anacheza na hamu hiyo kali ya kudhibitisha watu kuwa wamekosea.

“Lazima umwambie vizuri. Atakuwa tishio kwa sababu anacheza kwa kujiamini sana.”

Wakati Bruce anaogopa fomu ya Toney, anafurahishwa na matarajio ya kuongoza klabu ya mji wake kwenye nusu fainali ya kwanza ya kombe la ndani katika miaka 15.

Uchambuzi: Brentford vs Newcastle United.

Bosi wa Toon aliongeza: “Ninaitarajia. Tunayo nafasi nzuri ya kufika nusu fainali ya kombe hili, kwa hivyo wacha tufurahie changamoto yake na tuone ni wapi tunaweza kwenda.

Bosi wa The Bees Thomas Frank amezidisha presha kwa Newcastle, na kuiita kama timu pendwa kwa mchezo wa robo fainali.

Alisema: “Kuna wachezaji wengi katika timu yetu ambao wana ndoto kubwa na wanataka kwenda Ligi Kuu, kwa njia moja au nyingine.

“Newcastle ni kilabu kikubwa. Bado kuna vilabu vingine vichache ambavyo ni vikubwa kidogo kuliko sisi lakini tutafanya kila kitu kushinda mchezo.

Je, Ulijua?

Mara ya mwisho timu hizi kukutana katika Kombe la Ligi kati ya Bretford na Newcastle ilikuwa mwaka 2001 mwezi Septemba huko St James ‘Park, na Newcastle ilishinda 4-1 katika dakika za nyongeza na Craig Bellamy alifunga hat-trick wakati wa muda wa nyongeza.

Hii ni robo fainali ya kwanza ya Kombe la Ligi kwa timu ya Brentford baada ya mechi 153 kwenye mashindano, ambapo ni mechi nyingi zaidi zilizochezwa kabla ya kucheza kwenye mechi yao ya kwanza ya robo fainali katika historia ya mashindano.

Newcastle wametolewa katika mashindano mara saba kati nane katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Ligi na waliifunga Notts County mwaka 1975-76.


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

16 Komentara

    Newcastle ni chama kikubwa

    Jibu

    Mapema tuu kwa Newcastle

    Jibu

    Mechi ya kibabe sana hii

    Jibu

    Mechi kali san sio ya kukosa meridian bett ni moto

    Jibu

    Mechi ya kukata na shoka hii

    Jibu

    Mechi kali

    Jibu

    Mambo hayo

    Jibu

    Mechi ya tarii hii

    Jibu

    Mapema tuu kwa Newcastle

    Jibu

    Itakuwa sio powah

    Jibu

    Mechi kali

    Jibu

    Mechi mzur

    Jibu

    Newcastle idhihirishe umwamba wake kwenye hii mechi

    Jibu

    Dk 90 tu maana mpra siku hz autabrk

    Jibu

    Mechi kali

    Jibu

    Uchambuzi umekaa poa sana

    Jibu

Acha ujumbe