Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya brazil Ronaldo siku ya Jumamosi alikuwa kwenye mazungumzo na klabu ya Cruzeiro klabu yake ya kwanza kucheza mpira wa kulipwa kuhitaji kuinunua.
Ronaldo ambaye alianza kucheza kwenye timu ya kikosi cha kwanza cha Cruzeiro mwaka 1993 akiwa na miaka 16 tu, pia aliweza kufanikiwa kuichezea timu hiyo michezo 58 huku akifunga magoli 56 na kufanikiwa kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kwenda kushiriki michuano ya kombe la Dunia iliyofanyika Marekani.

“Tunakazi kubwa ya kufanya, niliwaomba mashabiki waweze kujumuika na timu kwa kwenda uwanjani sababu itatupa nguvu na kutuweka pamoja, tunakazi kubwa na shauku ya kuifanya Cruzeiro kuwa bora tena.” Alisema De Lima
Inatarajia kuwa Ronaldo atalipa kiasi cha Brazil reais 400 milioni ambapo sawa na 161 billion kwa pesa ya kitanzania na kuongoza kwa umiliki wa hisa nyingi kwenye klabu hiyo, awali alifanikiwa kununua klabu ya Hispania Valladolid ambayo inashiriki ligi ya daraja la pili kwa kiasi cha 30 million euros.
Fanya wiki yako iwe ya ushindi mkubwa ndani ya kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo wa BURST THE BANK🔥🤑 ni moja kati ya mchezo pendwa unaowapa wachezaji mamilioni kila siku. Kwa dau dogo unashinda zaidi.


