Mchezaji wa kimataifa wa Algeria, Sofiane Lokar amefariki dunia baada ya kupata mshtuko wa moyo uwanjani alipokuwa akicheza siku ya Krismasi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alizimia akiwa na kikosi cha timu ya daraja la pili ya Algeria, Mouloudia Saida.
Lokar alifariki kutokana na mshtuko wa moyo alipokuwa akiichezea Mouloudia Saida ya Algeria
Inadaiwa na Super Haber ya Uturuki kwamba Lokar alijijeruhi katika dakika ya 26 ya mechi dhidi ya ASM Oran kufuatia kugongana na kipa wa timu yake.Lokar alitibiwa jeraha na kisha akaruhusiwa kurejea dimbani.
Lakini dakika tisa tu baadaye, katika dakika ya 35, Lokar alianguka ghafla sakafuni.
Wahudumu wa afya walikimbilia eneo la tukio, lakini pamoja na jitihada zao za dhati hakuweza kuokolewa na kwa huzuni aliaga dunia.
Ripoti zinaonyesha kuwa Lokar jeraha la kwanza lilikuwa kichwani, lakini alipitishwa akiwa fiti kuendelea kabla ya umauti kumpata.
Lokar alikuwa nahodha wa Mouloudia Saida na inasemekana alifunga ndoa wiki iliyopita tu.
Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.


