NBA; Irving Ni Moto Mkali!

Songombingo za kugoma kuchanja chanjo ya Covid-19 zimemfanya akose baadhi ya michezo kwenye NBA. Lakini, Kyrie Irving ni wa moto…

Wakati huu ambao James Harden ameondoka Brooklyn Nets na kujiunga Philadelphia 76ers, ule utatu mkuu wa Nets (Harden, Irving na Durant) umevunjika. Hii hainamaana Nets wanataabika, hapana, kazi inaendelea.

Nets walikuwa uwanjani alfajiri ya leo wakichuana na Orlando Magic katika muendelezo wa NBA. Huu ni mchezo ambao, Irving ameendelea kuonesha ubora wake kila anapokuwa uwanjani. Safari hii, nyota huyo amepachika jumla ya pointi 60 (rekodi kwenye maisha yake ya kucheza kikapu) na kuchagiza ushindi wa pointi 150-108.

Huu unakua ni ushindi wa 4 mfululizo kwa Nets ambao wanaonekana kurejea kwenye ubora wao. Kwingineko viwanjani, Grizzlies wameondoka na ushindi vs Pacers (135-102), Heat wameifunga Pistons kwa pointi 105-98 huku Suns wakiwaacha na maumivu wenyenji wao –Pelicans kwa matokeo ya pointi 131-115.


SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI

Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.

liverpool, Liverpool Kila Mtu Ashinde Mechi Zake., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe