NBA: Lakers na Houston Washindwa Kutamba.

Bado hali ni tete kwenye NBA msimu huu wa 2020/21. LeBron James na James Harden wameshindwa kutamba kwenye mechi zao jana usiku.

LA Lakers walikuwa uwanjani wakipimana nguvu na Trail Blazers. Lakers walijikuta wakiambulia kipigo cha pointi 115-107.

Wachezaji wa Lakers wakichuana na Trent (Trail Blazers)

Huu ni mchezo wa pili kwa Lakers kupoteza katika msimu huu wa NBA. Licha ya kwamba LeBron James alipachika pointi 29 na kutoa pasi 6 za magoli, haikutosha kuwazidi nguvu Damian Lillard (pointi 31) na Gary Trent Jr (pointi 28).

Kwingineko kunako michezo ya NBA. Houston Rockets walijikuta wakiangukia pua mbele ya Denver Nuggets.

Uhodari wa James Harden haukutosha kuwaangusha Nuggets ambao waliibuka kidedea kwa ushindi wa pointi 124-111.

Harden aliisaidia Rockets kupata pointi 34, alitoa pasi 8 za magoli na alicheza mipira 6 iliyokufa.

Nikola Jokic akipambana na wachezaji wa Houston Rockets.

Kwa upande wa Nuggets, Nikola Jokic aliibukwa kinara baada ya kumaliza mchezo kwa matokeo ya ‘triple double’ – alifunga pointi 19, alitoa pasi 18 za magoli na alicheza mipira 12 iliyokufa.

Matokeo mengine ya michezo iliyochezwa Jumatatu hii:

Atlanta Hawks 128-120 Detroit Pistons, Memphis Grizzlies 116-111 Brooklyn Nets, Utah Jazz 110-109 Oklahoma City Thunder.

Mchezo wa kukata na shoka utachezwa leo usiku ambapo Milwaukee Bucks watachuana na Miami Heats.


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?

SOMA ZAIDI

21 Komentara

    Nouma Sana

    Jibu

    Hatari san

    Jibu

    Duuh ni shida

    Jibu

    Lakers wameshukaaaaa

    Jibu

    Lakers mmeniangusha sana chama langu

    Jibu

    Lakers vipi tena jaman

    Jibu

    Daah mipango sio matumizi sikitiko kwa lakers

    Jibu

    NBA ya msimu huu inaonekana itakuwa ya ushindani sana, Ngoja tuone

    Jibu

    Mambo yamebadlka kila mtu anataka kuwa juu

    Jibu

    Lakes walinde hadh yao nba

    Jibu

    Lakers msimu huu mbona wanatuangusha wamebanywa

    Jibu

    Mambo motooo

    Jibu

    Duu sio poaa msimu huu

    Jibu

    Wamauwanza msimu vibaya

    Jibu

    Hatari sana

    Jibu

    Sio mchezoo

    Jibu

    Siku hazilingani

    Jibu

    Lakers Mbona hvyo

    Jibu

    Duuh hatr sanaa

    Jibu

    Lakers wanamaliza vibaya

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.