Yanga Wahamisha Nguvu Shirikisho

BAADA ya kutolewa kwenye michuano ya Klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Al Hilal ya Sudan, Uongozi wa Yanga umefunguka kuhamisha nguvu yao kwenye michuano ya Shirikisho.

Yanga ilipoteza mchezo wa pili wa michuano hiyo dhidi ya Al Hilal kwa tofauti ya mabao 2-1 mechi iliyochezwa mjini Khartoum nchini Sudan.

Kikosi cha Yanga tayari kimerejea Dar leo jumatatu kikitokea nchini Sudan kikiwa na msafara wa wachezaji 25 pamoja na viongozi.

Akizungumza baada ya kutua nchini, Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said amesema “Kikubwa tunawashukuru sana wachezaji kwa kujituma kwao kwani walijitoa kwa asilimia zote lakini haikuwa bahati yetu.

“Bado tuna nafasi ya kuiwakilisha taifa kwenye michuano ya kimataifa hivyo kwa sasa tunageukia ligi pamoja na hayo mashindano ili tuweze kufanya vizuri huko.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.