Waandamizi Wamfurahisha Kocha Simba

BAADA ya kuingia hatua ya makundi ya michuano ya Klabu bingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amefurahishwa na viwango vya wachezaji waandamizi ndani ya kikosi hicho.

Simba iliingia hatua ya makundi baada ya kuiondosha Primeiro De Agosto ya nchini Angola kwa jumla ya mabao 4-1.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mgunda alisema “Kwanza tunamshukuru Mungu kwa kumalizika salama kwa mchezo.

“Pia wachezaji wangu hasa wale waandamizi ambao waliifanya kazi yangu kuwa nyepesi baada ya kufuata maelekezo ambayo niliwaelekeza.

“Wachezaji hao ni pamoja na Clatous Chama, John Bocco na Jonas Mkude ambao walifanya kazi yangu ambayo ilikuwa ngumu kuwa nyepesi.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.