FA Cup: Middlesbrough Waifungasha Vilago Man United

Timu ya Manchester United ilitolewa na timu ya Middlesbrough kwenye michuano ya FA Cup ikiwa ni raundi ya nne siku ya Ijumaa usiku, baada ya kupigiana mikwaju ya penalti.

FA Cup: Middlesbrough Waifungasha Vilago Man United

United ambao wananolewa na kocha Ralf Rangnick walipata bao la kwanza kupitia kwa mchezaji Jadon Sancho baada ya Christiano Ronaldo kukosa penalty kipindi cha kwanza cha mchezo lakini Matt Crooks wa Middlesbrough aliisawazishia timu yake dakika ya 64 ya mchezo hivyo kufanya ubao usome 1-1 baada ya dakika 90.

Licha ya kuutawala mchezo United walishindwa kupata matokeo na kutolewa kwenye matuta baada kupigiana peanti 7-8 baada ya Anthony Elanga kugongesha mpira kwenye besela.

Sasa matumaini ya Man United kwa sasa yamesalia kwenye Ligi ya Mabingwa ambayo inatarajiwa kuendelea Februari 15 hatua ya 16 bora.

Leo kuna michezo mingine inaendelea ya FA Cup ambapo Chelsea, Tottenham, Brentford Everton West Ham na nyingne zitaendelea na raundi ya nne.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.