Fury Awapiga Mkwara Joshua na Wilder

Bondia wa Uingereza Tyson Fury amewambia Deontay Wilder na Anthony Joshua kwamba wasahau kuhusu kuvunja rekodi yake ya kutopigwa.

Bingwa huyo wa miaka 33 wa WBC ambaye amezichapa mara mbili na Wilder huku akiibuka na ushindi sasa yupo tayari kumaliza ubishi na maneno dhidi ya Wilder huko Las Vegas mwezi Oktoba 9, wakati Joshua anatetea mataji yake ya IBF, WBO na WBA Super dhidi ya Oleksandr Usyk siku ya Jumamosi ijayo.

Ushindi kwa wote wawili utaweka pambano lao ambalo linasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mchezo wa ndondi, ambalo lilibuma mwanzoni mwa mwaka huu baada ya Wilder alipotaka pambano la tatu na Gypsy King.

Lakini Fury anasisitiza kuwa hatapigwa kamwe kabla ya kutundika glavu zake.

Katika mahojiano na The overlap ya Gary Neville, alisema: “Sijawahi kupoteza pambano. Sidhani nitashindwa pambano, hapana. Sidhani nitafanya hivyo.

“Sidhani kuna mtu yeyote huko anayeweza kunipiga.”


MKWANJA NJE NJE NA DISCO FUNK

Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe