Nyota mashuhuri wa Uingereza Anthony Joshua na Tyson Fury watapigania mikanda yote minne ya uzani mzito katika Mashariki ya Kati katika pambano ambalo ulimwengu umekuwa ukitamani.

Joshua Dhidi ya Fury Kufanyika Saudi Agosti 7 au 14

Na Hearn aliiambia Sky Sports Jumanne kwamba pambano hilo la kukata na shoka litafanyika mwezi Agosti 7 au 14.

Alisema pia kwamba mabondia wote wote walikuwa na furaha kuwaamini Wasaudi kwa sababu tayari ‘walitimiza kila ahadi zao’ kwa pambano la Joshua dhidi ya Andy Ruiz mwaka 2019.

Bado hakuna tangazo rasmi ambalo limetolewa lakini Hearn alidokeza wiki iliyopita kwamba mpango huo ulifanywa.

Alisema: “Pambano hilo [Joshua vs Fury] limekwisha pangwa na utapata tangazo hivi karibuni.”

Pambano hilo la mwezi Agosti litakuwa la kwanza katika makubaliano ya mapigano mawili, na pambano la pili linatarajiwa kufanywa mwishoni mwa 2021.

Imeripotiwa pia kwamba pambano hilo linaweza kutoa kiasi cha pauni milioni 500, huku Joshua na Fury wakikubali kugawana 50/50.

Fury hajapoteza katika mapambano 31 ya kitaalam, na kasoro yake pekee ni sare ya kutatanisha dhidi ya Deontay Wilder mwaka 2018, pambano ambalo wengi waliona alishinda.

Wakati huo huo, Joshua ana rekodi ya 24-1, na kupoteza kwake kulikuwa kwa kushangaza mikononi mwa Ruiz mwaka 2019.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Joshua, Joshua Dhidi ya Fury Kufanyika Saudi Agosti 7 au 14, Meridianbet

CHEZA HAPA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa