Tetesi za soka leo Jumatano Mei 26, 2021 zinasema:-

Tetesi zinasema, Kocha wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino anaangalia uwezekano wa kurejea katika klabu yake ya zamani ya Tottenham.

Tetesi zinasema, Hata hivyo, Spurs wanafanya mazungumzo na kocha mkuu wa Ubelgiji na meneja wa zamani wa Everton na Wigan Roberto Martinez, 47, wakati harakati za kumsaka atakayechukua nafasi ya Jose Mourinho zikiendelea.

Tetesi zinasema, Wolves wamejiandaa kumuuza kiungo wao Ruben Neves kwa pauni milioni 35 ili kupata pesa ya kukijenga kikosi chao kwa ajili ya kocha yeyote atakayechukua nafasi hiyo kufuatia kuondoka kwa Nuno Espirito Santo.

Tetesi za soka - PhilipeTetesi zinasema, Wolves hata hivyo hawatalazimika kumuuza Neves, 24, ambaye amekuwa katika klabu hiyo tangu mwaka 2017, lakini watasikiliza ofa yoyote kama itaiwezesha kukijenga upya kikosi chao.

Tetesi zinasema, Mchezaji nyota wa Brazil Philippe Coutinho, 28, atakuwa miongoni mwa wachezaji 10 walioorodheshwa kuuzwa na Barcelona katika dirisha la usajili la mwisho wa msimu huu.

Tetesi za soka - RobinTetesi zinasema, Barcelona na Manchester City ni miongoni mwa klabu zinazomtaka kiungio wa kati wa klabu ya Atalanta Mjerumani Robin Gosens, 26.

Tetesi zinasema, United wamekubali kusaini mkataba na mlinda mlango wa Aston Villa Muingereza Tom Heaton, 35, kwa uhamisho huru mwezi ujao.

Tetesi zinasema, Tottenham na Everton wanataka kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 28, kwa pauni milioni 40.

Tetesi za soka zahaTetesi zinasema, Mshambuliaji wa Arsenal Mbrazili Willian, 32, anataka kurejea katika kikosi cha Chelsea – ikiwa ni chini ya miezi 12 baada ya kuihama klabu hiyo aliyokaa nayo kwa miaka saba.

Tetesi zinasema, Mlinzi wa Villarreal Pau Torres, 24, amekataa kujadili kuhusu tetesi zijazomuhusisha na kuhamia Manchester United msimu huu, kabla ya mchezo wa Jumatano wa fainali za Europa dhidi ya United.

Tetesi zinasema, Chelsea huenda wanataka kumuuza kiungo wao wa kati Muingereza Callum Hudson-Odoi,mwenye umri wa miaka 20, huku akitarajiwa kwenda Borussia Dortmund . Dortmund pia wanaweza kuangalia uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa safu ya mbele wa Leeds United Mbrazili Raphinha, 24.


BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa