Euro 2020: Mashabiki wa Denmark Ruksa! Wales HAPANA

Kuelekea hatua ya 16 bora kunako mashindano ya Euro 2020, mchezo wa Denmark vs Wales utachezwa jijini Amsterdam – Uholanzi.

Japokuwa furaha na burudani nzima ya soka ni uwepo wa mashabiki viwanjani, mchezo wa Denmark vs Wales utashuhudiwa na mashabiki wa Denmark pekee.

Uholanzi imeruhusu mashabiki wa Denmark kuhudhuria kwenye mchezo huo kama tu, wataingia na kuondoka nchini humo ndani ya masaa 12. Licha ya kuwa Denmark ipo kwenye orodha ya nchi salama kwa mujibu wa vigezo vya Uholanzi linapokuja suala la Covid19, raia wanaoingia nchini humo wanapaswa kukaa karantini kwa siku 10.

Wales ni miongoni mwa nchi ambazo hazipo kwenye orodha ya nchi salama na hivyo mashabiki wa timu hiyo hawatoruhusiwa kuingia Uholanzi kushuhudia mchezo wao wa hatua ya 16 bora kunako Euro 2020.

Nafasi ya kukosa kushuhudia mchezo wao nchini Uholanzi, haiwazuii kuangalia mchezo wa robo fainali endapo watafanikiwa kufikia hatua hiyo. Julai 3, mchezo wa robo fainali utachezwa pale Baku.


USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao.
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

Acha ujumbe