Klabu ya Bayern Munich imethibitisha kumalizana na klabu ya Juventus kwenye uhamisho wa mlinzi wake wa kimataifa kutoka nchini Uholanzi Matthijs de Ligt.

Matthijs de Ligt ameigharimu klabu ya Bayern Munich kiasi kinachokadiliwa €70million huku kiasi hicho kinaweza kuongeza €10milioni zaidi, ikiwa klabu hiyo itafanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Ujerumani.

Bayern Munich, Bayern Munich Wathibitisha Kumsajiri Matthijs de Ligt, Meridianbet

De Ligt ni zao la klabu ya Ajax, na akiwa na miaka 19 alifanikiwa kuvaa kitamba cha unahodha kwenye mchezo wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya, kabla ya kununulia na klabu ya Juventus.

“Nina furaha kubwa kuwa mchezaji wa klabu hii bora, Bayern Munich ni klabu yenye mafanikio ndani ya Ujerumani, pia moja ya klabu yenye mafanikio ulaya na duniani.

Nilihisi upendo wa pekee kutoka kwenye menejimeni, kocha na bodi tangu mwanzo, hicho ndicho kilicho nishawaishi mimi. Licha ya yote FC Bayern ni klabu yenye malengo makubwa. Nina furaha kuwa sehemu ya historia ya klabu ya  Bayern.” De Ligt alisema

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa