BAADA ya kutoonekana kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Yanga, kiungo wa Simba Sadio Kanoute, Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema nyota huyo ni mgonjwa.

Mchezo huo wa ligi ulipigwa jana jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar ambapo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Kanoute, Kanoute Augua Ghafla!, Meridianbet

Mabao ya mchezo huo yalifungwa na Augustine Okrah dakika ya huku bao la kusawazisha la Yanga likifungwa na Stephane Aziz Ki dakika ya 45.

Mgunda alisema “Kwanza tunamshukuru Mungu mchezo umemalizika salama, mchezo huu ni mgumu kuliko michezo mingine.

“Kanoute aliumwa ghafla usiku na kupelekea kumuondoa kwenye kikosi kutokana na ugonjwa alioumwa akiwa kambini.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa