Kanoute Kukosekana Kariakoo Derby.

Kiungo wa klabu ya Simba raia wa Mali Sadio Kanoute atakosekana katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga utakaopigwa muda mchache kuanzia sasa katika dimba la Benjamin Mkapa.kanouteTaarifa kutoka ndani ya Klabu ya Simba zinadai mchezaji huyo ameumwa ghafla na kumfanya kukosekana katika mchezo huo ambapo litazibwa na kiungo Jonas Mkude ambae atacheza sambamba na Mzamiru Yassin katika eneo la katikati la Simba.

Kiungo Kanoute ambae amekua mhimili mkubwa katika eneo la katikati katika kikosi cha Simba hivo kukosekana  kwake katika mchezo wa leo dhidi ya Yanga inaweza kua pengo kubwa katika mchezo huo wa watani wa jadi.kanouteSadio Kanoute amekua akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara tangu ajiunge klabuni hapo lakini amekua msaada mkubwa kwa klabu hiyo pale anapokua timamu kimwili.

Acha ujumbe