Yanga watawakaribisha Mtibwa Sugar katika dimba la Benjamin William Mkapa kumenyana katika mchezo wa nne wa ligi kuu ya NBC Tanzania bara.

Timu ya wananchi baada ya kushinda mchezo wake wa hatua ya awali wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Zalan ya Sudani kusini leo hii wanajitupa uwanjani kukipiga na klabu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro.

yangaMtibwa Sugar wanakwenda kucheza na Yanga huku wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu huku wananchi wakiwa nafasi ya tatu huku wakiwa wamelingana alama wote wakiwa wana alama saba hivo mchezo huo unaenda kua wa kusisimua zaidi kwani ni vita ya nani apande juu ya mwenzake kwani atakaepoteza mchezo huo basi ni wazi atashuka na mwingine atapanda kwenye msimamo.

Huku kocha msaidizi wa klabu ya Mtibwa Sugar Awadh Juma Maniche ameeleza “kua wamejipangaa zaidi kuelekea mchezo hua kwani hawajapoteza mchezo na wapinzani wao hawajapoteza mchezo na kueleza atakaekua vizuri atashinda mchezo huo na suala historia halina nafasi katika mchezo na kusisitiza wako tayari kwa asilimia mia moja kupambana”.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa