Michael Zorc ametupilia mbali uvumi unao endelea juu ya staa Erling Haaland kuihama klabu ya Borussia Dortmund na kusema Dortmund ina mpango wa muda mrefu na nyota huyo.

Haaland ameendelea kufurahia maisha yake soka katika ligi ya Bundesliga baada ya kujiunga na Borussia Dortmund akitokea klabu ya Salzburg mwezi Januari mwaka huu na amekuwa anahusishwa na kujiunga na vilabu kama Real Madrid, Manchester United pamoja na Juventus.

Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 20 hivi karibuni alishinda tuzo ya Golden Boy 2020, amekuwa mchezaji mwenye kasi zaidi kufunga magoli 15 katika Champions League katika historia ya michuano hiyo baada kufunga magoli mawili kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya Club Brugge siku ya Jumanne.

Haaland ambaye ni raia wa Norway amefunga magoli 10 katika michezo saba ya Bundesliga msimu huu na kufunga magoli 17 katika mashindano yote msimu 2020-21 yakijumuishwa magoli sita katika Champions League.

Ikiwa Haaland anaendelea kuvivutia vilabu mabalimbali vya Ulaya Zorc ameweka bayana kuhusu hatima ya mchezaji huyo akiwa na mkataba wenye thamani ya €75m (£67m) ambao utafanya kazi mpaka mwaka 2022.

“Nafurahi pale ninapoona Haaland anahitajika na timu nyingi hii inamaana kwamba anacheza vizuri wote tunafanya kazi nzuri,” Zorc aliwaambia maripota kuelekea mchezo wa Jumamosi wa Bundesliga dhidi ya Cologne.

“Sitakiwi kusema kitu chochote kwa mameneja wengine, kwa sababu tuna mipango ya muda mrefu na Erling.

Tangu ajiunge na Dortmund mwanzoni mwa 2020, Haaland amefunga magoli 33 katika michezo 31 kwa miamba hiyo ya Ujerumani.

Haaland aweka wavuni magoli 23 katika michezo 22 ya Bundesliga akiwa na Dormund ambao wapo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama moja katika michezo nane.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa