Mshambuliaji wa Togo Emmanuel Sheyi Adebayor amedai hatatoa msaada wowote baada ya kukosolewa kwa kutokuwa mkarimu kusaidia wakati huu wa janga la virusi vya Corona. Mastaa wengi wa soka wametoa msaada kwa watu walio katika mazingira magumu katika nchi zao ili kuwasaidia kutokana na hali mbaya iliyopo kwa sasa ulimwenguni.
Lakini Adebayor nyota wa zamani wa Arsenal FC, Manchester City, Tottenham Hotspur na Real Madrid anafikiria tofauti. Nahodha huyo wa zamani wa Togo kupitia video zinazozunguka kwenye mitandao ya kijamii aliwajibu wakosoaji wake na kusema hakuleta ugonjwa huo mbaya nchini kwao.
“Ninafanya kile ninachotaka kufanya, ninakula kile ninachotaka kula na hii ni muhimu zaidi. Baadaye, kutakuwa na watu ambao watanikosoa kwa ukweli kwamba sikufanya msaada wowote huko Lome.”-Adebayor

“Lakini inaonekana kwamba mimi ndiye niliyeleta virusi vya corona huko Lome (nyumbani). Ni bahati mbaya sana, ndio watu wa nchi yangu.”
kuhusina na kinachofanywa na mastaa wenzake wanaosaidia nchini kwao?
Adebayor:
“Unaweza kunilinganisha na Didier Drogba, unaweza kunilinganisha na Samuel Eto’o, lakini kwa bahati mbaya mimi sio Didier Drogba, mimi sio Samuel Eto’o. Mimi ni Emmanuel Sheyi Adebayor na siku zote nitafanya kile ninachotaka kufanya.”


David pere
Nikweli kabisa hamfiki hata kidogo
Ester
Kufanya msaada si kijitangaza Ila kujitolea tu
Theonestina
Haswaa
Neema juma
Duu
felister
kutoa msaada ni uamuzi wa mtu