Kuna baadhi ya mambo unahitaji roho ngumu kuyafanya katika soka na kama una roho nyepesi hakika utabaki kujilaumu tu , ipo ivi mwanaume wa kweli huwa hajutii maamuzi yake na kujilaumu ni zaidi ya kujidharau ukiamua kuua ua tu alafu potezea ndivyo wanaume tulivyo , mwanaume haogopi kufa maana tunaishi huku tumekufa hela tunaipata ukiwa nusu maiti . Jose Mourinho alimtema Juan Mata na kumtemea Man Utd hakujali mtasema nini , Ferguson hakujutia kumpiga Beckam na kiatu na kumuuza juu , roho ya raisi wa Real Madrid Perez ni ya kiume haswa kuwauza Cloudio Makelele na Mesut Ozil wala hakufikiria mara mbili.

Wakati mwingine tuache taaluma zifanye kazi yake ujuaji nao sio mzuri kabisa , Mourinho alimuuza Juan Mata maana hakumuona katika stahili yake anafaa na alijua Mata hana muda mrefu katika soka la ushindani , licha ya uwingi wa assists na magoli pale Chelsea Jose aliona mbali . Juan ni kiungo mshambuliaji au kiungo wa kulia , Mata ni mtamu anapokutana na timu zizonacheza na mpira sio watu ambazo kwa sasa ni chache sana . Mourinho sio mjinga na hata Oleguna sio mjinga wanajua kabisa Mata sio wa aina hii ya sasa , hakuna tofauti kati ya Mata na Ozil ni wale wale wakati dunia ikizidi kuondokana na matumizi ya namba 10 wa asili wao bado wapo.
Mesut Ozil alipitia wakati mgumu chini ya Unai Emery maana kocha hakutaka mchezaji ambaye ili awe mzuri lazima muwe mnashambulia , lazima utakua na utindio wa ubongo wakati wenzako wana akina Kelvin De Bryune , Bruno Fernandez , Delle Alli , Fabregas , Christian Eriksen , Wijnaldum , Tonny Kross au Luca Modrick kama viungo washambuliaji wewe una Ozil . Mpira unakua mgumu tena wa mahesabu makubwa huwezi kua na wachezaji ambao hawezi kua mzuri nyuma ya mpira , mpira unahitaji raia wenye nguvu na mahesabu kuna kitu kinaitwa Tactical Peridiozation , watu wanabadilishana majukumu winga anaweza kua kiungo mshambuliaji na maisha yanaenda . Kama una mchezaji ambaye hana madhara akiwa nusu yake ni wazi unamiliki lawama ndio maana Unai akagoma kupangiwa , sio Ozil hata Isco tu hata James Rodriguez ndio maana kila mtu hamtaki.

Mesut ni bonge la mchezaji tena mzuri sana lakini haendani na wakati hata Arteta moyoni analijua hilo , embu mfikirie David Silva na umri wake tena mtizame De Bryune mpe wakati wako Luca Modrick je unaanzaje kurudi kwa Ozil au Mata ? . Turudi nyuma kidogo Frank Lampard alikua kiungo mshambuliaji kwa asili embu kumbuka harakati zake uwanjani , siku timu ikihitaji kujilinda basi Frankie alikua mtu au mtizame Iniesta ni wazi hawezi kukaba lakini anajua kucheza katika nusu yake . Hata leo mwite mshabiki mwenye akili wa Arsenal achague kati ya Ozil na Cazorla uone atakwambia nani , Ozil ni mrembo kuanzia sura macho yake nywele zake uchezaji wake hata mwanamke wake naye ni mrembo tu.
Hakuna ubaya kwa Ozil lakini muda unamtupa mkono na anakwenda mdogo mdogo na yeye amekataa kuendana na wakati , baadhi ya wajerumani walimlaumu baada ya kutoka hatua ya makundi kombe la dunia waliamini katika uchezaji wake anahusika kwa namna fulani , amini nakwambia kwa soka la saivi lazima useme jamaa hajitumi uwanjani . Mpira wa saivi ni zaidi ya mahesabu ndio maana Liverpool magoli yanatoka pembeni tena kwa mabeki , huwezi kua mtu anayekupa chaguo moja tu.


Povel
Thnks meridian bet kwa update za michezo na burudani
Theckla
Asante kwa taarifa
David Pere
Kwanini Sasa awe bingwa wa misaada alafua aachwe na wakati hiyo sio kweli
Shafii
Makala nzuri
Lydia Emmanuel Magoti
Tarifa nzuri meridian nawakubali
Gabriel
Nice update 👍# meridianBetTZ
isha
Duuh mambo mengine uzushi bhuanaa
Ester jackson
Hakuna ubaya kwa Ozil lakini muda unamtupa mkono na anakwenda mdogo mdogo sana hivyo amejiachia sana kimichezo
Elika
Safi sana ozil
Samiah
Ozol mtu mmbaya
Magdalena
Duh ozil noma
Omary lukumbi
Ozil mchezaj anae heshimika Germany ila tuu hata club aliyo kuwepo kwa sasa haimpi nuru ya kutazamwa zaid kama alivyo miaka ya huko nyuma
Tahiya
Ozil ni mchezaji mzuri sana ila ni mzembe sana akiwa uwanjani na iyo inapelekea kiwango chake kushuka
Mwanaidi
Ni kweli Ozil ni bonge la mchezaji lakini haendani na wakati
Khadija
Ozil mtu mbaya#meridianbettz
Rehema
Ozil namkubali sn
Adelta
Safi sana ozil
Neema hassan
Asante kwa habari#meridianbettz
warda
Namuonaga Ozil ni mchezaji Asie Na bahati#Meridianbettz
Hope mwaikuka
Imeeleweka hyo
Emmy cleopa
Ahsante kwa makara
Devotha
Asante kwa taarifa
felister
Mimi macho yako tu Ozil
Johnmary joel
Kabisaa ozil nimekukubali sanaa#meridianbett
Issa
Ozil vizuri na bonge la streka
Caroline
Muda unamtupa mkono Ozil lakini .lakn anakwenda mdogo mdogo
lombo
asante meridianbet kwa update
Salma
Mko vizuri kwa taharifa
Njiku
Mesut ozil nifundi wa mpira na anauwezo mkubwa sana akiwa kwenye secta yake ila mambo madogo madogo ya kujilekebisha tu hasa kwenye upande wa ukabaji ila kwa soka la uingereza ni mchaka mchaka anatakiwa kucheza ligi yeyote Spain hata levante,sevilla nk
Dorophina
Talent player
Ernest
Napata shida kidogo kuona kusema kiwango cha Ozil kipo chini sana maana muda mwingi amekosa nafasi ya kuonyesha makali yake dimbani
Hamidu
Fudi wa mpira #meridianbettz
Genia Sikaluzwe
Ni fundi Sana wa mpira
Sadick
Kwa umri wa Ozil si rahisi kubadilika labda angekuwa na Kocha dizaini ya Guardiola angeweza. Asubiri kustaafu akale maisha na mrembo wake#meridianbettz
Sabrina
Maoni:Ozil jeshii
Frank Patrick
Super playmaker
Furahav
Habari nzuri.
Zeiyana
Mesut ozil namkubali sana nimkalimu na anapenda kujitolea kama ivyo pongezi sana kwake
Tatu
Asante kwa taarifa