Mshambuliaji wa Simba Moses Phiri amesema kuwa anajisikia kuwa na amanai mara baada ya kufanikiwa kufunga bao katika michezo yake miwili mfululizo aliyocheza ya ligi kuu ndani ya timu hiyo.

Phiri alifanikiwa kufunga mabao mawili katika michezo miwili mfululizo dhidi ya Geita Gold ukiwa mchezo wa kwanza huku akifunga bao la pili katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

Simba, Moses Phiri: Nitaifungia Simba Magoli ya Kutosha, Meridianbet

Phiri alisema kuwa anajisikia mwenye furaha kuisaidia timu kupata matokeo lakini kubwa zaidi kwa upande wake ni kuifunga mabao 2 ambayo kwa kiasi kikubwa yamempa amani ya kuendelea kupambana kwaajili ya kuipa mafanikio zaidi Simba.

“Nafurahi kwanza kuona Simba tumefanikiwa kufanya vizuri katika michezo yetu ya mwanzo kwa kuwa nafahamu ni jinsi gani Simba ilikuwa kwa msimu uliopita ambapo timu kuna baadhi ya vitu ilivikosa ambapo msimu huu tunahitaji kuona tunavipata.

“Pili kuifuingia Simba katika michezo mfululizo kwangu hii inanijenga kwaajili ya kuhakikisha kyuwa napamabana ili niweze kufunga ambao mengine mengi zaidi ndani ya klabu hiii,” alisema mshambuliaji huyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa