HATIMAYE kocha wa Simba Zoran Maki amefunguka kuwa alikuwa anafahamu kuwa mshambuliaji wake Dajen Georgejevic kuwa angefunga katika mchezo dhidi ya Kagera kutokana na nafasi nyingi ambazo zilikuwa zikitengenezwa kushindwa kutumiwa jambo ambalo lilimfanya kumuingiza uwanjani akiamini kuwa angefunga.

Dejan katika michezi miwili ya ligi kuu akiwa na Simba amefanikiwa kufunga bao moja huku katika michezo yote hiyo hakuna hata mchezo mmoja ambao ameanza yote akiwa amenzia benchi.

Zoran, Kumbe Zoran Alitabiri Mzungu Angetupia!, Meridianbet

Kocha Zoran alisema kuwa alifahamu kama Dejan angeweza kufunga bao mara baada ya kuona nafasi nyingi zikitengenezwa bila kutumiwa vizuri jambo ambalo baada ya kumuingiza mshambuliaji huyo na akafanikiwa kufunga.

“Washambuliaji wangu walitengeneza nafasi nyingi sana za kufunga lakini wakatumia nafasi chache sana,hata wakati nawaza kufanya mabadiliko ya kumuingiza Dejan nilihisi kuwa angefunga kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutumia nafasi.

“kwa sasa nachojivunia ni amefunga kwa kuwa inamuondolea presha aliyokuwa nayo naamini kuna ubora mkubwa tutaupata kutoka kwake,”alisema kocha huyo.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa