Unamjua Nwankwo Kanu?

Leo katika kolamu hii ya Nyota ya Afrika nakuja na mchezaji wa zamani wa Nigeria. Ni Nwankwo Kanu,lakini katika majina kiutani wengine tunamtambua kama Papilo. Jina la Papilo ni la utani kama ilivyo kwa wachezaji wetu wa kitanzania Kuitwa Nungunungu,Cotton juice mweni,Sonso na mengine Mengi. Nwanko ni mzaliwa wa Owerri Agosti mosi 1976, kutoka kabila la Igbo,moja ya makabila makubwa nchini Nigeria kama ilivyo kwa Hausa na Yoruba. Ana kimo chenye urefu wa mita 1 na sentimeta 97 (1.97) sawa na futi 6 na inchi 6.Jamaa ni mrefu ni sentimenta tatu pekee zinamfanya asifikishe meta mbili.

Nwankwo Kanu

Alianza kucheza soka katika klabu ya Iwuanyanwu Nationale nchini Nigeria mwaka 1992 hadi 1993. Baada ya kuwa na kiwango bora katika michuano ya kombe la dunia kwa vijana wa chini ya miaka 17 mwaka 1993 nchini Japan. Waholanzi wang’amua kipaji cha Kanu aliyekuwa akicheza kama mshambuliaji.Alijiunga na miamba ya kiholanzi Ajax Amsterdam mwaka 1993 hadi 1996. Akiwa Ajax alipata kubeba ubingwa wa Uefa champions league mwaka 1995, alicheza kama mchezaji aliyetokea benchi katika mtanange dhidi ya Ac Milan waite Rosaneri.

Baada ya kutamatika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika Atlanta nchini Marekani mwaka 1996, Klabu ya Inter Milan ilimnunua Kanu toka Ajax na kujiunga na miamba mingine ya soka la Italia waite Nerrazuri. Baada ya kujiunga na Inter ilimpasa kusubili kuitumikia klabu hiyo kwani aligundulika kuwa na tatizo la moyo. Alifanyiwa upasuaji wa Moyo November 1996 na hakurejea klabuni hadi April 1997. Kisa hiki ndicho kilichofanya hadi sasa Kanu awe na mfuko wa kuchangia wagonjwa wa masuala ya Moyo na pia kuwa hospital ya matibabu ya Moyo. Waluguru wanasema “Ambe lilimfika jaah”. Tatizo lake limeleta utatuzi kwa jamii na nchi ya Nigeria.

Kwa kipindi cha miaka mitatu (1996 hadi 1999) alicheza mechi 12 pekee na kufunga goli moja akiwa na Nerrazuri. Aliamua kubadili upepo na kwenda kujiunga na Miamba ya soka la uingereza klabu ya Arsenal fc. Aliitumikia klabu ya Arsenal,West Bromwich Albion na Portsmouth akiwa ligi ya Uingereza.Alimaliza maisha yake ya soka akiwa na vijana wa ‘The pompy” sambamba na Mnigeria mwenzake John Utaka aliyewahi kupata wakati mgumu mbele ya Boniface Pawasa,lakini pia alikuwa na Mghana Sulley Ally Muntari,Msenegal Abdulaye Faye na Waafrika wengine hapo Portsmouth.

Moja ya miamba aliyopata kucheza nao akiwa Arsenal ni Marc Overmas, Ray Parlour, Denis Bergkhamp na nyota kutoka Afrika kama Lauren Emtama Mayer wa Cameroon.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.