Nguli wa mchezo wa tenesi duniani Roger Federer ambae ametangaza kustaafu mchezo huo siku kadhaa nyuma inaelezwa atacheza mchezo wake wa mwisho ijumaa hii.

Nyota huyo anatarajiwa kucheza kwenye mashindano ya watu wawili wawili kwenye kombe la Laver huku akimtaja mpinzani wake wa muda mrefu Rafael Nadal kama rafiki wa ndoto zake.

roger federerRoger anatarajia kuungana na wachezaji kama Nadal,Novak Djokovic, pamoja na muingereza Andy Murray, Wachezaji wengine wa tenesi maarufu kama Big Four ambao wataiwakilisha timu ya ulaya kwenye uwanja wa O2 Arena wanaweza wasiwepo kutokana na utimamu wa kimwili.

Nyota huyo ambaye ameshinda Grand slam 20 alitangaza kustaafu mchezo wiki iliyopita baada ya kusumbuliwa na majeraha ya goti kwa mrefu ambayo yamekua yakimueka nje ya uwanja mara kwa mara.

Federer ametangaza kushiriki michuano ya kombe la Laver inayohusisha wachezaji wawili wawili wa tenesi ijumaa hii huku akiungana na magwiji mbalimbali wa mchezo huo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa