Tetesi zinasema, Chelsea wanataka kumsajili mchezaji wa safu ya kulia na nyuma wa Inter Milan na Morocco Achraf Hakimi,22 ambaye amekuwa akinyatiwa na Paris St-Germain.

Tetesi zinasema, Kocha wa zamani wa Liverpool na Newcastle Rafael Benitez anagombea nafasi ya ukufunzi iliyoachwa wazi Everton.

Barcelona wanatafakari uwezekano wa kumnunua winga wa Manchester City na England Raheem Sterling, 26, ambaye anaonekana kuwa mrithi mahiri wa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Ousmane Dembele,24, ikiwa hatasaini mkataba mpya.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tottenham wanafanya mazungumzo na winga wa Borussia Monchengladbach Mfaransa Marcus Thuram – kabla ya kumsajili msimu huu wa joto.

Tetesi zinasema, Kipa wa Uhispania David de Gea, 30, anatarajia kusalia Manchester United msimu ujao.

Tetesi zinasema, Arsenal wamejiunga na Liverpool, Tottenham na Manchester United katika kinyang’anyiro cha kumsaka mlinzi wa Brighton na England Ben White, 23.

Tetesi zinasema, Roma wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa kati wa Uswizi Granit Xhaka, 28, kutoka Arsenal.

Kiungo wa kati wa RB Leipzig raia wa Austria Marcel Sabitzer, 27,ambaye awali alihusishwa na tetesi za kuhamia Tottenham, anataka kuondoka klabu hiyo ya Bundesliga na huenda akanunuliwa kwa karibu euro milioni 15 msimu huu.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Burnley wamefikia mkataba mpya na kocha wao Sean Dyche, 49, ambaye anatarajiwa kurejea dirisha la uhamisho litakapofunguliwa msimu huu.

West Ham wameongeza juhudi za kumsajili Jesse Lingard kwa mkataba wa kudumu kutoka Manchester United baada ya kiungo huyo wa kati wa Uingereza kutemwa katika kikosi michuano ya Ulaya.

Porto wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsaini kiungo wa kati wa Liverpool na Serbia Marko Grujic baada ya kuwa katika klabu hiyo msimu uliopita kwa mkopo.

Leicester City wanamenyana na Wolfsburg na Lyon katika jaribio la kumsaini winga wa Bournemouth Mholanzi Arnaut Danjuma,24.

Tetesi zinasema, Leeds United wanapania kumsajili kiungo wa kati wa Fulham Harrison Reed, 26, msimu huu wa joto.

Tetesi zinasema, Winga wa Newcastle Muingereza Jacob Murphy, 26, anatakiwa na Galatasaray.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Kocha wa Roma Jose Mourinho amewasiliana na mshambulizi wa Torino na Italia Andrea Belotti, 27, ambaye anaongoza orodha ya wachezaji anaotaka kuwasajili.

Mlinzi wa Uhispania Sergio Ramos, 35, ana matumani ya kuanza mazungumzo ya mkataba na Real Madrid na yuko tayari kuongeza mkataba wake wa sasa.

Deportivo Alaves wanataka kusaini mpya mkataba wa mkopo wa winga wa Manchester United na Uruguay Facundo Pellistri,19.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa