Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Bayern Munich wanaweza kumuuza mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski msimu wa joto ikiwa hata saini mkataba mpya, mkataba wa sasa unakamilika mwezi Juni 2023.

Wawakilishi wa Cristiano Ronaldo wameiambia Manchester United kwamba mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 36 anapania kuondoka Old Trafford msimu wa joto ikiwa klabu hiyo itashindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Tetesi zinasema, Atletico Madrid haitamruhusu mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 34, ambaye anahusishwa na uhamisho wa Aston Villa, kuondoka mwezi Januari.

 

Suarez Athibitisha Kusalia Atletico kwa Msimu Mwingine

Barcelona wamepiga hatua katika mazungumzo kumhusu mlinzi wa Chelsea Andreas Christensen, 25, huku kandarasi ya mchezaji huyo wa Denmark ikitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Manchester United itamruhusu kiungo mshambuliaji Jesse Lingard kuondoka mwezi Januari ikiwa klabu italipa ada ya mkopo ya £3.5m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye kandarasi yake huko Old Trafford inakamilika msimu wa joto.

Rais wa Lille Olivier Letang anasema klabu hiyo ya Ufaransa haitafungua hata mlango wa kujadili kumuuza mlinzi wa Uholanzi Sven Botman, 22 huku Newcastle United na AC Milan zikiwa na nia ya kumsajili.

Arsenal wameongeza kasi ya kumsaka kiungo wa Juventus Arthur Melo, huku The Gunners wakitumai kumsajili Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu.

Juventus wamechukizwa na kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kukataa ofa ya kuwahama Waitaliano hao kutoka vilabu vya Uingereza na Uhispania.

 

Aaron Ramsey

Tetesi zinasema, Bayern Munich wako tayari kukabiliana na Manchester United katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Uswizi na Borussia Monchengladbach Denis Zakaria, 25.

Tetesi zinasema, Paris St-Germain wanauhakika kwamba kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane, 49, ataiongoza Parc des Princes msimu ujao.

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa na Arsenal Thierry Henry yuko katika kinyang’anyiro cha kuwa kocha wa Bordeaux atakapojiondoa kama mkufunzi wa Montreal Impact mwezi Februari.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe