Wachezaji 5 Wanaongoza kwa Kadi Nyekundu

Wachezaji wengi hupewa adhabu ya kadi nyekundu chache sana kwenye soka, lakini wapo ambao maisha ya adhabu yamekua ya kawaida kwao. Kadi nyekundu ni chaguo la mwisho kabisa la waamuzi kumudu mchezo iwapo ukiwa hauendi sawa. Mara nyingine adhabu hiyo hutoka kwenye matukio ya bila kukusudia lakini yanakua hayavumiliki. Kuna baadhi ya wachezaji tukio la kadi nyekundu limekua la kawaida saana kwenye maisha yao ya soka na huona sawa tuu kupata kadi nyekundu kiasi cha kufanya makosa ya kudhamiria. Kadi nyekundu ni tukio linalo leta ahueni kwa wachezaji wa timu pinzani na huumiza zaidi timu iliyo adhibiwa.

Leo tunakupa list ya wachezaji  5  wanao ongoza kwa kupewa kadi nyekundu katika historia ya soka la kimataifa.

  1. Paolo Montero (21)
Paolo Monterlo

Raia huyu wa Urugwai ndie anae ongoza kwa kua na rekodi ya kadi nyekundu nyingi zaidi kwenye historia ya ligi kuu ya Italia Serie A kwa kupewa kadi nyekundu mara 21 katika maisha yake ya soka. Montero alisikika akisema “muda mwingine unatakiwa kufanya chochote ili kushinda na hii ndio asili yangu siwezi kubadirika”

  1. Alexis Ruano Delgado (22)
Alexis Luano Digalo akimpiga muamuzi kibao

Beki wa kati mwenye asili ya Uhispania anaefahamika kwa hasira zake na konde lake alilo mwangushia Mario Mandzukich, Alexis amepewa kadi nyekundu 22 kwenye historia yake ya soka la kimataifa.

  1. Sergio Ramos (25)
Sergio Ramos

Ukitaja rekodi za wachezaji watukutu utakua na kosa kubwa bila kumtaja Sergio Ramos. Muhispania huyo amepata jumla ya kadi nyekundu 25, huku kwenye ligi kuu ya uhispania pekee akipata kadi nyekundu 20. Sergio pia anaongoza kwa kadi nyekundu kwenye michezo inayowakutanisha wao na washindani wao Barcelona maarufu kama El Classico.

  1. Cryil Rool (27)
Syril Rool

Wachambuzi wa soka wanasema Rool ni hatari hata kwenye maisha ya kawaida, Rool ametambulika zaidi kwa rafu zake za hatari za kuruka mateke kwa wapinzani anao kutana nao huku akipata kadi nyekundu  zaidi ya 27.

  1. Gerardo Bedoya
Gerard Bedoya mwenye jezi nyekundu

Anatambulika kama mchezaji mkorofi kuliko wote walio wahi kutokea kwenye historia ya mpira wa miguu. Mlinzi huyo wa kati mwenye asili ya Colombia amepewa kadi 46 nyekundu kwenye historia yake ya soka. Bedoya mara zote huonekana kama amechanganyikiwa anapokua uwanjani. Kocha wake wa timuya vijana aliyewahi kumfundisha miaka dadhaa katika timu ya vijana ya Colombia amesema “watu hawabadiriki”

4 Komentara

    Gerard Bedoya mwenye jezi nyekundu
    Anatambulika kama mchezaji mkorofi kuliko wote walio wahi kutokea kwenye historia ya mpira wa miguu ila wamemsahau ballotel

    Jibu

    Duuuh

    Jibu

    Gud update

    Jibu

    Majanga hayo

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.