Dejan Avunja Mkataba na Simba.

Dejan Georgijevic mshambuliaji wa Simba amethibitisha kuachana na klabu hiyo baada ya kuposti kwenye mtandao wake wa kijamii baada ya muda mfupi wa kuwepo klabuni hapo.

Siku kadhaa nyuma kumekua na stori ya kutokua na maelewano na baadhi ya wachezaji ndani ya klabu hiyo na hii imeonekana siku kadhaa baada ya kutokua na maelewano na mchezaji mwenzake wa klabu hiyo raia wa Ghana Augustine Okrah katika mchezo wa kirafiki huko Visiwani Zanzibar.

dejanKumekua na baadhi ya taarifa kua mchezaji huyo amekua akilalamikia uongozi kua wachezaji wenzake wanamnyima pasi uwanjani kitu ambacho ameshindwa kukivumilia kutokana na tabia hiyo ya baadhi ya wachezaji wenzake.

Dejan Georgijevic ameeleza sababu ya kuvunja mkataba na klabu hiyo ni kutokana na timu hiyo kutokutimiza makubaliano ya kimkataba waliyoingia baina yao hivo kuamua kusitisha mkataba huo.

dejanDejan Georgijevic mshambuliaji huyo aliepata umaarufu sana siku za karibuni baada ya kutambulishwa katika siku ya Simba Day na “Neno la Mlete Mzungu” likawa maarufu sana baada ya pale na kumfanya mshambuliaji huyo kupata umaarufu,kutambulika na kupendwa na Watanzania kabla ya leo kutangaza kuachana na timu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.