Nabi Awaomba Mashabiki kwa Mkapa

KUELEKEA kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal, Kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kutoa sapoti kwa wachezaji.

Al Hilal wanatarajia kuwasili nchini leo alhamis kwa ajili ya mchezo huo ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar saa 10:00 jioni.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema: “Maandalizi yamekamilika kwa asilimia 90 mpaka sasa tunachosubiria ni kuwasili kwa wageni wetu.

“Kocha Nabi amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Mkapa siku hiyo kwa ajili ya kuwapa sapoti wachezaji wetu.

“Amesema hili niwafikishie ili waweze kuja kwa wingi kwani wao ni wachezaji wa 12 uwanjani hivyo itaongeza nguvu na morali kwao.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.