Klabu ya Al-Hilal kutoka nchini Sudan wameahidiwa kupewa hela kwa kila mchezaji, endapo watashinda mchezo wa leo dhidi ya Yanga na kufanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Viongozi wa Al-Hilal wamewaahidi wachezaji wa timu hiyo kila mmoja atapatiwa kitita cha Dola 5,000 endapo watawafunga yanga na kufuzu hatua ya makundi ya CAFCL.
Taarifa kutoka kwa Mwandishi wa Habari wa nchini Ghana MickyJr iliandika kuwa.
“Bodi ya wasudani hao imewaahidi kila mchezaji kiasi cha Dola 5,000 kama wataweza kuwaondoa Yanga na Kufuzu hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa”
Mchezo wa Kwanza utachezwa Leo majira ya Saa 16:00 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, na kisha Yanga watasafiri kurudiana na AL-Hilal nchini Sudan, ambapo mshindi wa jumla atafuzu kuingia hatua ya makundi.

