Wonder Kid Peter Banda, ambaye ni winga wa klabu ya Simba baada ya kuwa nje kwenye michezo kadhaa ya timu yake, huku akiikosa safari ya kucheza mechi ya ugenini dhidi ya De Agosto ya Nchini Angola, kutokana na majeraha ameweka wazi maendeleo yake.
Winga huyo kijana raia wa Malawi aliumia kwenye mchezo wa kirafiki na timu ya Malindi ya Zanzibar, na hivyo kulazimika kuwa nje mpaka leo ambayo imemfanya akose mchezo dhidi ya Kipanga, Dodoma Jiji na Mchezo wa Kimataifa Kesho nchini Angola.
Kupitia Taarifa yake aliyoandika kwenye Twitter Peter Banda alielezea maendeleo ya majeraha yake na kusema kuwa anaendelea vizuri.
“Njiani Kupona, Asante kwa meseji zenu za matumaini, nakuwa vizuri kila siku na nitarejea hivi karibuni kuwapa furaha kama kawaida. Kila la heri kwa Mnyama Simba SC Tanzania kwenye mchezo wa Ligi ya MABINGWA huko Angola.”
Peter Banda amekuwa na kiwango kizuri msimu huu, haswa kwa upande wa pembeni akiisaidia timu yake kupeleka mashambulizi kwa kasi na kuifanya kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC nyuma ya mahasimu wao Yanga SC.

