TFF imetoa ufafanuzi kwa ambayo yalikua yanaendelea mitandaoni juu ya kocha aliekaimu nafasi ya kocha mkuu ndani ya klabu ya Simba Juma Mgunda.

Kumekua na maneno yanaendelea kwenye mitandao ya kijamii kuanzia jana juu ya kocha Juma Mgunda mara tu ya kutangazwa atakaimu nafasi ya kocha mkuu ndani ya klabu ya Simba ikielezwa kocha huyo hana leseni ya kuweza kusimama kama kocha mkuu kwenye benchi la ufundi kwenye timu hiyo kama ilivyoelezwa hapo hapo mwanzo na kudaiwa kocha wa Simba queens atajiandaa kuelekea Malawi kuongoza timu hiyo.

tffBaada ya uvumi huo shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limetoa tamko na kutaja majina ya makocha wenye leseni za Caf ndani ya nchi hii na kocha huyo wa zamani wa Coastal Union ya Tanga akiwa miongoni mwao akiwa na leseni ya Caf diploma A hivo ana hadhi na vigezo vya kuingoza timu hiyo kwenye michezo ya kimataifa.

Baada ya taarifa hii imeweza kuondoa ukakasi na maneno yaliyokua yanaendelea juu ya mwalimu Juma Mgunda.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa