Hakika NBA msimu huu mambo ni moto! Sio kwenye Eastern wala sio Western Conference, kote mambo ni mazito. Utah Jazz na LA Lakers, vita ya kusaka ubingwa inaendelea kuwa ya moto.
Jazz walikuwa uwanjani kuchuana na Milwaukee Bucks katika mchezo ambao Jazz wameendelea kuwa bora zaidi, ushindi wa pointi 129-115 unaendelea kuwaeka Jazz kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Western Conference.

Katika kuhakikisha Bucks hawafui dafu, Jazz walimaliza mchezo kwa wachezaji wao wanne kupachika zaidi ya pointi 25 kila mmoja – Rudy Gobert (pointi 27), Joe Ingles (27), Donovan Mitchell (26) na Jordan Clarkson (25).
Licha ya Giannis Antetokounmpo kujitahidi kupachika pointi 29 na kucheza mipira 15, haikuwasaidia Bucks kuepuka kipigo cha 2 mfululizo na Jazz kuibuka na ushindi wa 6 mfululizo.
Kwingineko katika NBA, LA Lakers wameendelea kufanya vizuri msimu huu. Hii ni baada ya kupata ushindi wa 7 mfululizo kwa kuwafunga Memphis Grizzlies kwa pointi 115-105.

Kurejea kwa Antony Davis (AD) kuliongeza chachu kwenye timu hiyo. AD alipachika jumla ya pointi 35 na kucheza mipira 9 iliyokufa. Sambamba na AD, swahiba wake – LeBron James alipachika pointi 28, alicheza mipira 9 iliyokufa na kutoa pasi 8 za magoli.
Matokeo ya michezo ya NBA iliyochezwa Ijumaa usiku:
Charlotte Hornets 120-114 Minnesota Timberwolves, New York Knicks 109-91 Washington Wizards, San Antonio Spurs 125-114 Atlanta Hawks, Dallas Mavericks 143-130 New Orleans Pelicans, Los Angeles Clippers 125-106 Chicago Bulls, Detroit Pistons 108-102 Boston Celtics, Denver Nuggets 97-95 Oklahoma City Thunder, Portland Trail Blazers 129-110 Cleveland Cavaliers na Orlando Magic 123-112 Sacramento Kings
Unaweza kuvuna mkwanja mrefu kadiri uwezavyo kupitia mchezo wa Gold n Rocks kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Ni rahisi! Vigezo na masharti, kuzingatiwa.
Caroline
N.B.A kumenoga
Magdalena
Lakers nawaaminia
Dorophina
Lakers wanavita sio ya kitoto
Adelta
Lakers kwa sasa wako moto sana
Sania
Mhh ushindani ni makubwa sana
Rahma
Lakers wako vizuri
Sarah
Lakers nawakubala
Sadick
Ubora wa Ligi ya NBA umetawala duniani kwa muda mrefu kwasasa. Na wiki ijayo mashabiki watarejea uwanjani kuleta hamasa zaidi
Mwanahamisi
Lakers wako vizuri
Lydia Emmanuel Magoti
Kumenoga
Neema juma
Vita ya kusaka ubingwa ni moto.wako vzr lakers
Hopemwaikuka
NBA kumenogaa
Venerose
Mambo ni 🔥🔥🔥
Ernest Kimeru
Ngoja tuone
Angelina
Tunasubiri mashabiki
warda
Lakers wako poa sana