Ahmed Ally: Tutachunga Yasitokee ya Msimu Uliopita.

Afisa habari wa klabu ya Simba Ahmed Ally amesema msimu watajitahidi yasitokee yaliyotokea msimu uliomalizika katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy.

Ahmed Ally amezungumza wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa marudiano dhidi ya klabu ya Premiro De Agosto ya Angola, Akizungumza Afisa huyo  maandalizi ya kuelekea mchezo huo amekumbusha kua hawajasahau yaliyotokea msimu ulioisha dhidi ya Jwaneng.ahmed allyMsimu uliomalizika Simba walishinda magoli mawili kwa bila dhidi ya klabu ya Jwaneng Galaxy ya Bostwana ugenini lakini mambo yalibadilika katika dimba la Benjamin Mkapa baada ya kupinduliwa meza nyumbani na kujikuta wakitupwa nje ya michuano hiyo, Hivo Afisa huyo amesisitiza wanakumbuka kilichotokea na hawatadharau mechi na watacheza kama hawakupata matokeo mechi ya kwanza.

Simba watarudiana na klabu ya Premire De Agosto wikiendi hii baada ya kushinda mabao matatu kwa moja hivo ni kama wameingiza mguu mmoja hatua ya makundi lakini Ahmed Ally amesisitiza wanakwenda kucheza mchezo huo kwa heshima na kujituma zaidi ili kuepuka kilichotokea katika msimu uliopita.Pia Afisa habari huyo alielekeza namna ya kupatikana kwa tiketi za mchezo huo na kuwataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao na kuiona ikifuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.